Nini kinatokea Papa anapofariki? Pia utaratibu wa kumpata Papa Mpya

Kasomi

JT Founder
Nini hutokea baada ya kifo cha Papa Francis?
GpCy-sVXUAA3TN-.jpeg

Ulimwengu na haswa waumini wa Kanisa Katoliki limetumbukia katika majonzi baada ya kutangazwa kuwa kiongozi wao Papa Francis amefariki akiwa na umri wa miaka 88.

Nini kinatokea?

Mazishi ya papa kwa kawaida yamekuwa tukio la kipekee na lenye mambo mengi, lakini Papa Francis hivi majuzi aliidhinisha mipango ya kufanya utaratibu mzima usiwe mgumu.

Mapapa waliotangulia walizikwa katika majeneza matatu yaliyotengenezwa kwa mvinje, risasi na mwaloni.

Papa Francis amechagua jeneza rahisi la mbao lililowekwa zinki.

Pia amefutilia mbali utamaduni wa kuuweka mwili wa Papa kwenye jukwaa lililoinuliwa - linalojulikana kama ‘catafalque’ - katika kanisa la St Peter Basilica kwa ajili ya kutazamwa na umma.

Badala yake, waombolezaji wataalikwa kutoa heshima zao huku mwili wake ukisalia ndani ya jeneza, kifuniko kikiwa kimetolewa.

Francis pia atakuwa Papa wa kwanza katika zaidi ya Karne moja kuzikwa nje ya Vatican.

Atazikwa katika Basilica ya St Mary Major, mojawapo ya mabasili kuu manne ya Papa huko Roma.

Nini kitafuata?

Vatican sasa ipo katika kipindi rasmi cha maombolezo kitakachodumu kwa siku 9.

Kifo cha Papa kimethibitishwa na Chamberlain wa Kanisa

Alifanya hivyo kwa kuita jina la Papa Francis mara tatu, na baada ya kutopata jibu, akaarifu Kanisa na umma kuhusu kifo chake.

Chamberlain pia amefunga rasmi chumba cha Papa — hapo zamani watu walikuwa wakivamia na kupora.

Pia, amepanga ivunjwe pete ya Papa Francis kama ishara ya mwisho wa utawala wake na mwanzo wa kipindi cha "sede vacante" — yaani kiti kitupu cha Papa.

Lakini hayo hayakufanyika wakati Papa Francis alichaguliwa.

Kwa nini sasa?

Kwa sababu Papa wa mwisho, Benedict XVI, alijiuzulu kwa sababu za kiafya mwaka 2013 — alikuwa wa kwanza kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 600.

Kwa sasa, mazishi ya Papa Francis yanapaswa kufanyika kati ya siku ya nne na ya sita baada ya kifo chake. Katika kipindi hiki, mwili wake utawekwa wazi kwa umma katika Basilika ya Mtakatifu Petro kwa heshima na sala kutoka kwa wageni.

Mamilioni ya waombolezaji na waumini wa kanisa Katoliki wataelekea Roma, na zaidi ya makardinali 250 kutoka duniani kote watawasili pia. Baada ya mazishi, Papa Francis atazikwa kwenye kaburi lililo chini ya Basilika hiyo.

Baada ya hapo, Makardinali watafanya uamuzi mkubwa: Kumchagua Papa mpya. Mchakato huu unaitwa "Papal Conclave", na lazima uanze kati ya siku 15 hadi 20 baada ya kifo cha Papa.

Katika Conclave, Makardinali hufungiwa katika Kanisa la Sistine, bila mawasiliano na dunia ya nje. Watapiga kura mara kwa mara hadi mgombea mmoja apate asilimia mbili ya tatu (2/3) ya kura. Ikiwa watapiga kura kwa siku 12 bila mafanikio, basi mtu atahitaji asilimia 51 tu ya kura ili awe Papa.

Tangu 1975, ni Makardinali 120 tu wanaoruhusiwa kushiriki, na lazima wawe na umri chini ya miaka 80. Kwa sasa kuna 140 wanaotimizi vigezo hivyo, hivyo 20 walio wachanga zaidi hawatashiriki.

Wakati wa kupiga kura, ulimwengu utakuwa ukitazama moshi kutoka kwenye bomba la paa la Sistine Chapel mara mbili kwa siku. Moshi mweusi — hakuna Papa. Moshi mweupe — Papa mpya amechaguliwa!

Atakapochaguliwa, atachagua jina lake la upapa, na atatangazwa kwa dunia kutoka kwenye roshani kuu ya Vatican.

Soma zaidi:

Papa Francis afariki akiwa na umri wa miaka 88, Vatican inasema
 

Similar threads

Back
Top