Advertise here

Polepole aitwa polisi kathibitisha taarifa anazotoa

Kasomi

JT Founder
1757922219069.jpg

Jeshi la Polisi Tanzania, lingependa kutoa taarifa kuwa lilifungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akitoa Humphrey Herson Polepole toka Julai 2025.

Tuhuma ambazo ametoa na anaendelea kuzitoa kulingana na jinsi alivyozielezea zinaashiria uwepo wa makosa ya kijinai na kwa mujibu wa sheria zinahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapo wasilishwa mahakamani.

Tuhuma hizo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya Kijamii.

Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo/ushahidi na vielelezo vitakavyo thibitisha tuhuma hizo ili kuwezesha hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na ndivyo utaratibu wa kisheria ulivyo.

Hivyo Jeshi la Polisi kupitia taarifa hii linaendelea kumwelekeza afike katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili aweze kutoa maelezo/ushahidi kuhusiana na tuhuma ambazo amekuwa akizitoa kwa umma kupitia Mitandao ya Kijamii.

Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania.
1757921946740.jpg
 
Back
Top