Kasomi
JT Founder
Google imeongeza Lugha mpya 24 zinazozungumzwa na watu zaidi ya Milioni 300 katika Jukwaa lake la Tafsiri za Lugha 'Google Translate'. Idadi hiyo itafanya Lugha zilizopo ikiwemo Kiswahili kufikia 133
Inaelezwa kuwa kati ya Lugha zinazoongezwa, 10 zinatokea Barani Afrika. Kampuni hiyo imesema inalenga kusaidia wale ambao Lugha zao hazitambuliki katika Teknolojia nyingi
Mara kadhaa yamekuwepo malalamiko kuwa tafsiri za Lugha (Mfano Kiingereza kwenda Kiswahili) kwenye Google Translate zinaondoa maana halisi, na Kampuni hiyo imekiri Teknolojia yake sio kamilifu