Telegram itatoa taarifa za anwani ya IP na namba za simu za watumiaji wake kwa polisi

Kasomi

JT Founder
1727339403199.jpg

Telegram imebadili sera zake na sasa itakuwa inakabidhi anwani za IP na namba za simu za watumiaji na mashirika ya kutekeleza sheria kama kutakuwa na ombi halali la kisheria.

Mabadiliko haya yanakuja baada ya mamlaka za Ufaransa kumshtaki Mkurugenzi Mtendaji wa Telegram, Pavel Durov, kwa kuruhusu biashara haramu na kushindwa kuzuia na kudhibiti watumiaji.

Durov ametangaza kuwa timu yake imekuwa ikiondoa maudhui hatari na haramu kutoka kwenye Telegram. Sehemu ya Search pia imeboreshwa ili iwe vigumu kupata maudhui haramu. Telegram pia imeondoa sehemu ya ‘People’ Nearby’.

Mabadiliko haya ni sehemu ya kujibu changamoto zinazotokana na ukuaji wa haraka wa Telegram na ongezeko la idadi ya watumiaji.
 

Similar threads

Back
Top