JamiiTalk hulinda mazungumzo yako/yenu kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho

Kasomi

JT Founder
JamiiTalk hulinda mazungumzo yako/yenu kwa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho.

Hii inamaana kwamba ujumbe wa faragha hua katika yako na watu unao wasiliana nao hata JamiiTalk yenyewe haiwezi kuona wala kusoma.

Ujumbe wa faragha hufumbwa mwisho hadi mwisho. Hakuna mtu nje ya soga yenu, hata JamiiTalk yenyewe anaweza kusoma wala kuona.

Usalama wa JamiiTalk
Faragha na Usalama vipo kwenye damu yetu
Kutoka siku ya kwanza, tumebuni JamiiTalk ili ikusaidie uendelee kuwasiliana na marafiki, kushiriki maelezo muhimu wakati wa majanga ya asili, kuungana tena na wadau mbalimbali, kushiriki katika mijadala au kutafuta maisha bora. Baadhi ya matukio ya binafsi zaidi katika maisha yako hushirikiwa kwa kutumia JamiiTalk na ndiyo maana tumebuni ufumbaji wa mwisho hadi mwisho kwenye programu yetu.
Kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe, picha, video, ujumbe wa sauti, nyaraka za faragha hulindwa ili zisiingie kwenye mikono isiyofaa.

Utumaji Ujumbe wa Binafsi
Mfumo wa JamiiTalk wa ufumbaji wa mwisho hadi mwisho hutumika unapomtumia ujumbe mtu mwingine anayetumia JamiiTalk kwa PM.
Ufumbaji wa mwisho hadi mwisho huhakikisha kuwa ni wewe tu na mtu unayewasiliana naye mnaweza kusoma au kusikiliza ujumbe unaotumwa, na kwamba hakuna yeyote katikati, hata JamiiTalk yenyewe. Hii ni kwa sababu kwa kutumia ufumbaji wa mwisho hadi mwisho, ujumbe wako hulindwa kwa kufuli, na ni wewe na mpokeaji pekee mlio na ufunguo maalum wa kuufungua na kuusoma ujumbe huo. Haya yote hufanyika kiotomatiki: hakuna haja ya kuwasha mipangilio au kupanga soga maalum za siri ili kudumisha usalama wa ujumbe wako.

Hivyo kutumia JamiiTalk kuwasiliana kwa PM ni sehemu salama kabisa.
 
Hili napinga kwa asilimia 100% sidhani bwana Kasomi unajua maana ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho nikweli unaweza ahidi ya kwamba hamuwez kusoma PM ila mfano hacker wenye utaalamu watakapo fanikiwa kuingia katika mfumo kwa uzembe basi nirahisi sana kusoma

Mfumo huu hata telegram hawana maana halisi ya mfumo huu ji kuwa simu ya mtu hua server ya kuhifadhi data yake ambalo hii haiwezekani kwa forum
 
Hili napinga kwa asilimia 100% sidhani bwana Kasomi unajua maana ya ufumbaji wa mwisho hadi mwisho nikweli unaweza ahidi ya kwamba hamuwez kusoma PM ila mfano hacker wenye utaalamu watakapo fanikiwa kuingia katika mfumo kwa uzembe basi nirahisi sana kusoma

Mfumo huu hata telegram hawana maana halisi ya mfumo huu ji kuwa simu ya mtu hua server ya kuhifadhi data yake ambalo hii haiwezekani kwa forum
Asante kwa challenge.
Lakini kumbuka taarifa za mteja wetu (user) hua zipo encrypted hivyo hakuna mtu nje ya JT au JT wenyewe wanaweza access data au taarifa zozote kwa njia yeyote zaidi ya mtumiaji mwenyewe kutoa uwezekano wa mtu kuingia katika account yake.

mfano hacker wenye utaalamu watakapo fanikiwa kuingia katika mfumo kwa uzembe basi nirahisi sana kusoma
Naam, nakubaliana na wewe hilo hutokea hata kwa Mitandao mingine mikubwa lakini tunajitahidi kulinda hilo lisitokee.

Karibu sana mkuu
 
Back
Top