john achila mukumwa
Member
Tumia Maarifa Katika Kutenda Wema
Wema ni nini
Wema ni neno lenye maana kubwa katika jamii, likiwakilisha tabia njema na fadhili ambazo mtu anaweza kuzionyesha kwa wengine. Ni zaidi ya neno la kawaida; ni dhana inayohusisha mambo mengi mazuri yanayojenga jamii yenye upendo na mshikamano.
Katika muktadha wa kijamii, wema unadhihirika kupitia vitendo vya huruma na msaada kwa wengine bila kutarajia malipo au faida yoyote. Watu wanaoonyesha wema husaidia wale wanaohitaji, huwafariji walio na huzuni, na kuchangia kuboresha maisha ya wengine kwa njia mbalimbali. Kwa mfano, kutoa chakula kwa wenye njaa, kuwatembelea wagonjwa, au hata kutoa maneno ya faraja kwa wanaokabiliwa na changamoto. Yote haya ni matendo yanayodhihirisha wema.
Wema pia una uhusiano wa karibu na maadili na uadilifu. Mtu mwenye wema hufanya mambo kwa njia ya haki na yenye heshima, akijali hisia na ustawi wa wengine. Watu wa aina hii ni waaminifu, wanathamini utu wa kila mtu, na mara nyingi wanachukua hatua za kujenga mazingira yenye upendo na amani.
Wema pia ni msingi wa urafiki na mahusiano mazuri katika jamii. Watu wanapokuwa na wema, wanajenga urafiki wa kudumu unaotegemea uaminifu na msaada wa kweli.
Kwa upande wa kiroho, wema ni sifa ambayo dini nyingi zinahimiza. Katika Ukristo, kwa mfano, wema ni mojawapo ya matunda ya Roho Mtakatifu, na waumini wanahimizwa kuonyesha wema kwa watu wote.
Kwa ujumla, wema ni tabia muhimu inayofanya maisha kuwa bora zaidi. Inapotekelezwa na watu wengi, wema una nguvu ya kubadilisha jamii, kuondoa chuki, na kuleta amani. Katika ulimwengu wa leo, ambapo kuna changamoto nyingi, wema ni sifa inayohitajika zaidi kuliko wakati mwingine wo wote.
Ufafanuzi kuhusu kutumia maarifa katika kutenda wema
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa”.
Wema usiokuwa na maarifa bado haujakamilika. Ni kweli unaweza kufanya wema na nia yako ikawa ni njema, lakini wema huo usipoufanya kwa maarifa, huenda ukakuletea madhara hata wewe mwenyewe uliofanya huo wema.
Hebu tuangalie mtu mmoja katika biblia ambaye alifanya wema wake katika maarifa yote. Huyo ni yule Msamaria Mwema (Luka 10:30-35).
Luka 10:30 “Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. 31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.
32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.
33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, 34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akazitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. 35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa”.
Tunaona kuwa Msamaria huyu alipopita njiani na kukuta mtu amelala kando, hakukurupuka na kumpeleka nyumbani kwake, alale na watoto wake au ndugu zake. Badala yake, alimchukuwa na kumpeleka katika nyumba ya kulala wageni. Akiwa huko, huenda aliendelea na hatua nyingine za kuripoti habari yake katika vyombo vinavyohusika, ili kama ikiwezekana apate msaada zaidi wa kuwapata watu wa nyumbani kwake, au msaada zaidi wa huduma za hospitali.
Tujiulize: kwa nini Msamaria hakumpeleka nyumbani kwake moja kwa moja? Siyo kwa sababu hakuwa na huo uwezo, au labda ni mbali. La! Bali ni kwa sababu alitumia maarifa katika wema wake. Tukumbuke kuwa alikuwa hamjui yule mtu, hivyo kumchukuwa na kumpeleka nyumbani moja kwa moja, ingeweza kuwa hatari, kwa sababu huenda angekufa, na matatizo yakawa kwa yule aliyemsaidia. Au huenda si mtu mzuri, wakati wa kulala usiku angeweza kupata nafuu, huenda angeamka na kumdhuru yule aliyemsaidia. Hivyo, suluhisho la akili na hekima si kumpeleka nyumbani, bali katika nyumba ya kulala wageni.
Hali kadhalika na sisi tunapaswa tufanye wema wetu katika maarifa. Si kila anayehitaji msaada basi ni wa kumpatia kile anachokihitaji yeye, bali tunapaswa tupime namna ya kumsaidia kwa maarifa.
Mifano ya kutumia maarifa katika kutenda wema
1. Mtu usiyemjua akikuomba fedha
Mtu usiyemjua, akikuomba fedha ya hitaji fulani, ni vizuri usimpe hiyo fedha, bali umnunulie hilo hitaji lake na kumpatia.
2. Mtu usiyemjua akihitaji msaada wa malazi
Ukimkuta mtu usiyemjua yupo katika hali ya kuhitaji msaada wa kimalazi, usimchukue moja kwa moja na kumpeleka kwako. Jitahidi umtafutie mahali pa kulala, hususan nyumba ya kulala wageni,
angalau kwa siku moja, huku unaendelea kufuatilia taarifa zake na kuziripoti kwenye vyombo vinavyohusika. Ukishajiridhisha vya kutosha, ndipo unaweza kumhamishia kwako.
3. Mtu usiyemjua akikuomba nguo
Mtu usiyemjua akikuomba nguo, kama una uwezo, mnunulie nguo yake mpya. Usitoe ile ya mwilini mwako na kumpatia, kwa sababu shetani anaweza kuitumia hiyo kama mlango wa kukuletea matatizo maishani mwako. Lakini kama mtu unamjua au umejiridhisha kabisa na huna wasiwasi naye, unaweza kumpa moja kwa moja nguo inayotoka moja kwa moja mwilini mwako.
4. Mtu usiyemjua akikuomba lifti ya usafiri
Mtu usiyemjua akikuomba lifti ya gari, au pikipiki, au baiskeli, kama una uwezo mlipie nauli apande katika chombo kingine. Hiyo ni kwa sababu humjui mtu huyo ni nani, na hivyo ni rahisi kutumiwa na adui kuleta madhara yo yote kwako.
5. Mtu usiyemjua akikuomba chakula
Mtu usiyemjua akikuomba chakula kutoka katika sahani yako, usimpe kile chakula. Badala yake, mnunulie cha kwake binafsi, kwa sababu shetani anaweza kumtumia kama chombo cha kukuletea matatizo. Hiyo ni kwa sababu unaweza kumpa na kumbe kile chakula hakiendani na mwili wake, hivyo kikamletea madhara au hata kifo. Jambo hilo likitokea, linaweza kutafsiriwa kuwa umemuwekea sumu au dhara lolote, na kukuingiza wewe kwenye matatizo pasipo sababu yoyote.
Hivyo, ni lazima katika wema, kuweka na maarifa.
Kumbuka kuwa usiache kutenda wema, bali utende kwa maarifa.
Na hata katika mambo mengine yote mema unayoyafanya kwa mtu ye yote, hakikisha unayafanya kwa maarifa. Ndivyo biblia inavyofundisha.
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu, maarifa”.