Ochola12
New member
Ili mwanadamu awe timamu kiafya , Kijamii na Kiroho anapaswa kufanya mazoezi ili kuboresha mfumo wake wa Mwili ,Kuondoa mafuta na sumu zisizohitajika mwilini , kutengeneza nguvu pia Mazoezi yana faida nyingi kwa afya ya mwili na akili. Hapa kuna baadhi ya faida kubwa za mazoezi:
1. Mazoezi huimarisha afya ya moyo wa Mwanadamu, Mazoezi huimarisha moyo na kuzuia magonjwa ya moyo. Kupitia mazoezi Yanasaidia kuboresha mtiririko wa damu na kupunguza shinikizo la damu yani Low Blood pressure na High blood pressure
2. Kupunguza uzito , karne tulionayo miongoni mwa maradhi mabaya. yanayotupata ni uzito uliokithiri hivyo Mazoezi yanaweza kusaidia katika kudhibiti uzito kwa kuchoma kalori, ambayo ni muhimu katika kupunguza uzito hivyo jaribu kuwa na tabia ya kufanya mazoezi anza na mazoezi madogo , kama kuruka kamba, kuogelea, kukimbia na ya viungo
3. Mazoezi huimarisha misuli na kuongeza nguvu za mwili: Kwa kufanya mazoezi mara kwa mara, mwili hujenga nguvu na uvumilivu wa misuli hivyo nishati inayoleta nguvu hutengenezwa pamoja na mazoezi hayo inapaswa kuzingatia ulaji wenye tija ikiwemo Mboga za majani kwa wingi, Maziwa (Kuimarisha misuli), vyakula vya wanga , Protein (Hujenga mwili)
4. Mazoezi huimarisha afya ya mifupa: Mazoezi yanaweza kusaidia kuimarisha afya ya mifupa na kuzuia magonjwa kama osteoporosis. Yanasaidia pia kuboresha afya ya viungo.
5. Mazoezi huimarisha afya ya akili , Mazoezi ya kawaida yanaweza kusaidia kuboresha mood, kupunguza wasiwasi (Phobia) na kuboresha usingizi. Pia yanaweza kuongeza ufanisi wa akili na uwezo wa kukumbuka miongoni mwa watu wanaofikiri kwa haraka na ufanisi mkubwa ni wale wanaofanya mazoezi na kuzingatia kanuni za afya ikiwemo ulaji,Mapumziko, Hewa safi na kufanya kazi.
6. Mazoezi huimarisha Mfumo wa kinga Mazoezi yanaweza kuimarisha mfumo wa kinga, hivyo kusaidia mwili kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko ,Homa , Maradhi ya Moyo, Shinikizo la damu yani (High blood pressure na Low Blood pressure), Kisukari
7. Mazoezi huimarisha afya ya jamii: Kushiriki mazoezi katika vikundi au klabu kunaweza kusaidia kuimarisha uhusiano wa kijamii na kusaidia kujenga urafiki mpya, kupata uzoefu mpya , kuongeza mtandao wenye matokeo chanya kijamii na kiuchumi.
Ni muhimu kufanya mazoezi kwa kiwango kinachofaa na kulingana na uwezo wa mtu binafsi. Pia, ni vizuri kushauriana na daktari au mtaalamu wa afya kabla ya kuanza mpango wowote wa mazoezi, hasa kama kuna matatizo ya afya.kuna umuhimu, maelezo ya juu yanashauri kabla ya mazoezi ni vema ukafanye uchunguzi wa afya kwa upande wa moyo kwa kutambua maradhi kama Shinikizo la damu ili daktari aruhusu ufanye mazoezi kulingana na changamoto unayoipitia.