Mahusiano, Madeni Chanzo Cha Padri Nikata Kujiteka

Kasomi

JT Founder
1760733501244.jpg


Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limethibitisha kumpata Padre Camillius Nikata wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, ambaye alikuwa ameripotiwa kupotea tangu Oktoba 9, 2025 ambaye amepatikana akiwa salama katika mashamba ya Kijiji cha Mawa, kata ya Hanga, wilayani Namtumbo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amethibitisha kupatikana kwa Padri Nikata, ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) na kueleza sababu nne za kutoweka kwake ikiwemo msongo wa mawazo, mahusiano, maradhi pamoja na kucha kazi ya upadri.

Kamanda Chilya ameeleza sababu ya kwanza ya Padri Nikata kutoweka kuwa ni msongo wa mawazo kutokana na madeni mengi yaliyokuwa chini ya uwezo wake kubainisha kuwa upelelezi umebaini madeni hayo ambayo Padri huyo alikuwa anakabiliana nayo na kuonesha kwamba alishindwa kuyarudisha.

Sababu nyingine ni mahusiano ambapo Kamanda Chilya ameeleza kuwa Padri Nikata aliachwa na mpenzi wake aliyekuwa naye kwa muda wa miaka tisa na ambaye alikuwa anamhudumia kwa ghafama kubwa ambapo mwezi wa saba mpenzi wake huyo aliamua kuachana naye.

Ufuatiliaji wa polisi umebaini kuwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi Juni mpaka Septemba Kiongozi huyo wa imani alikuwa amemhudumia mpenzi wake huyo kwa zaidi ya Tsh milioni 39 akizitoa kwenye akaunti yake ya CRDB.

Sababu ya tatu huyo 'kujipoteza' kama alivyoeleza Kamanda Chilya ni maradhi ambapo Padre Nikata kwa muda mrefu alikuwa anasumbuliwa na presha ya macho na alifanikiwa kufanyiwa 'operation' ya jicho moja na sasa alikuwa anahitajika kufanyiwa 'operation' ya jicho la pili lakini alikosa fedha kutokana na matumizi makubwa ya kumtumia mpenzi wake huyo ambaye ana umri wa miaka 28 tu.

Kamanda Chilya ameeleza sababu ya nne ni kwamba Padri huyo aliamua kuachana kazi ya upadri kutokana na matatizo ya kiafya, sababu za kimahusiano, sababu za hali mbaya ya kifedha lakini hakupewa nafasi ya kusikilizwa na viongozi wake.
 
Back
Top