Advertise here

Maturity Kwa mwanaume sio kuoa au kuwa na mahusiano

Kasomi

JT Founder
Anaandika Emmanuel Minga

Maturity Kwa mwanaume sio kuoa au kuwa na mahusiano! Sio wote wameoa au wanamahusiano wako mature!

Maturity sio viwango vya madarasa ulivyosoma, Wala sio utimilifu wa malengo uliyowahi kujiwekea, na Wala sio umri au muonekano.

Ukomavu wa mtu unaonekana Kwa kupitia mtazamo wake, Namna anavyoweza kuyadhibiti na kuyatatua mambo yanayomkabili.

Mtazamo wa mtu ndio unaoonesha ukomavu wake,

Wewe unajichukuliaje? Unayakabili vipi matatizo yanayokukumba na unaishi vipi na wanaokuzunguka, vipi unafanyaje ukijua umekosea au umekosea, vp ukifanikiwa unakuwaje?

Kujitambua Kwako ndio kutaonyesha ni Kwa kiasi gani uko matured.

Kuna watu wanamahusiano na watu siojitambua ndio maana mahusiano Yao yanamisukosuko isiyo isha.

Kuna watu wanazani wameingia kwenye mahusiano kulelewa tu hawajui wajibu wao, hawajitumi Kwa chochote na Bado wanadai kupendwa.

Uzuri wa sura au umbo lako havina Msaada wowote kwenye mahusiano yako isipokuwa viwango vyako vya kujitambua.

Sura yako haimsaidii kitu huyo mkaka Wala umbo lako halimuongezei Hela, anahitaji mwanamke anayejitambua na aliye tayari kuwajibika kwenye mahusiano yake.

Brother umebahatika kumpata mdada anajitambua , tulia basi , tulia mtunze mtoto wa watu. Asije akaona na kujuta kuwa na mtu mzima mwenye mambo ya kitoto.

Ni kweli ni single mother lakini kuendelea kuangaika na wanaume unaonyesha Bado hujamature, kama hali yako ya kwanza imeshindwa kumtumza mwanamume uliyekuwa naye kwanini uendelee kuluka na wanaume? Badili mtazamo wako jiboreshe na pambana umtunze mwanao.

Usiwe mwanaume wa kukimbia majukumu, kuwa mwanaume wa kutegemewa.

Tunawatu wengi tunaowaona watu wazima lakini matendo Yao yanaonyesha kutokukua.

Na kuwa na mtoto, au kuwa na mwanamke au mwanaume hakumaanisha kwamba unajitambua! No !

kujitambua hakuji tu unahitaji kujifunza, nawapenda Sana watu wanaouliza maswali au wanaotafuta ushauri wa Namna Bora ya kufanya mambo Yao, Kwasababu huwezi kupata mbinu mpya bila kuzitafuta, Jifunze Kwa wengine waliofanikiwa na waliofeli pia.

Inatosha hapa, jitafakari na chukua hatua.

E.M✍️
 
Upvote 0

Similar threads

Back
Top