Kasomi
JT Founder
JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Martha Japhet (44) mkazi wa kitongoji za Mzalendo Kijiji cha Mawemelo kata ya Nyarugusu wilaya ya Geita kwa tuhuma za kumuua na kisha kumzika ndani mme wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Safia Jongo ametoa taarifa ya tukio na kumtaja marehemu ni Shabani Paschal (55) ambaye alikuwa ni mkulima na mchimbaji madini.
SACP Jongo amesema tukio hilo lilibainika Oktoba 16, 2025 majira ya saa 7 mchana kwani taarifa za tukio zilitolewa na watoto wa marehemu walioripoti kuwa baba yao haonekani nyumbani tangu siku ya Oktoba 11, 2025.
Amesema kabla ya taarifa hizo tayari walikuwa wamefanya juhudi mbalimbali za kumtafuta baba yao lakini hazikuweza kuzaa matunda ambapo mwanamke huyo alikamatwa na upelelezi ulianza mara moja.
Amesema baada ya mahojiano makali, mwanamke huyo alikiri kuwa marehemu ni mme wake, na kwamba tukio lilitokea Oktoba 11, 2025 majira ya saa tatu usiku baada ya mme kurudi nyumbani usiku.