Advertise here

Ongezeko la idadi ya laini za simu kwa ajili ya mawasiliano ya watu (P2P) zilizo sajiliwa

Kasomi

JT Founder
📌Ongezeko la idadi ya laini za simu kwa ajili ya mawasiliano ya watu (P2P):
1760903457309.jpg

Laini za simu za mkononi na mezani zilizosajiliwa kwaajili ya matumizi ya watu zimeongezeka kwa takribani milioni 6.5 katika robo ya mwaka iliyoishia Septemba 2025.

Ripoti ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano ya Septemba 2025 inaonesha kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia 7.1 kutoka laini milioni 91.7 Juni 2025 hadi kufikia laini milioni 98.2 Septemba 2025. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jumla ya idadi ya laini za simu kwa matumizi ya binadamu na mashine imefikia milioni 99.3 huku ikionesha kuwa wanaume wanaomiliki laini za simu ni milioni 50,457,144 na wanawake wakiwa milioni 47,708,505.

Umiliki wa laini za simu umekuwa msaada kwa kurahisisha shughuli za watumiaji wa huduma za mawasiliano kwaajili ya kuendesha biashara na kuwezesha ukuaji wa sekta nyingine kama afya, elimu na kilimo.
 
Back
Top