Advertise here

SENSA 2022: Idadi ya Watu Tanzania imefikia milioni 61,741,120

Kasomi

JT Founder
Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120.

Watu 59,851,347 wapo Tanzanzia bara na 1,889,773 Tanzania zanzibar.

Wanawake wapo 31,687,990 sawa na asilimia 51 ya watu wote na wanaume ni 30,530,130 sawa na asilimia 49 ya watu wote.

Kati ya mwaka 2012 hadi 2022, ongezeko la watu ni 19,812,197 sawa na asilimia 3.2

Tanzania bara, mkoa wa DSM unaongoza kwa watu nchini, wapo 5,383,728 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini, na mkoa wa pili ni mwanza wenye wakazi 3,696,872 sawa na asilimia 6.

Idadi ya mejengo ni 14,348,372 ambapo Tanzania bara yapo 13,907,951 na Zanzibar yapo 440,421

Vituo vya kutolea huduma za afya vipo 10067 ambapo zahanati zipo 7889, vituo vya afya 1490 na hospitali 688.

Upande wa shule, zipo 25,626 ambapo shule za msingi zipo 19,769 na shule za sekondari zipo 5857

Makadirio yanaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa na watu 67,962,097 na hadi kufikia mwaka 2050 idadi itafikia 151,252,429.
 

Similar threads

Back
Top