Advertise here

Hizi ndo Nchi ambazo Urais/ Rais hana nguvu kubwa kwenye Madaraka

Kasomi

JT Founder
No.1 China
Tuanze na huyu superpower

Wenda baadhi ya watu wanaweza wakawa wanafahamu na wengi wasiwe wanafahamu.

Ndivyo ilivyo Rais au cheo cha Urais China hakina nguvu kubwa sana kulinganisha na vyeo vingine kama Katibu mkuu wa chama cha kikomunisti au cheo cha mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya China.

Katika nchi za kikomunisti chama kinacho ongoza kina mamlaka makubwa ya kiuongozi katika nchi.

Nguvu za kiuongozi katika nchi hizi zipo zaidi chamani.

Mfano wa kueleweka zaidi ni aliyekuwa mwanamapinduzi na mwana mageuzi wa China Deng Xiaoping.

Deng katika historia ya uongozi wake toka 1978 mpaka kutamatika kwake hakuwahi kabisa kuwa Rais wala Katibu mkuu wa chama cha kikomunisti cha China lakini ndie aliyekuwa kiongozi mkubwa China.

Ki vipi ilikuwaje? Katika yale madaraka makubwa katika nchi za kikomunisti hasa chamani basi ni Katibu mkuu wa chama na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya Chama na Deng Xiaoping alikuwa mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya China.

Hivyo madaraka yake makubwa huyu mtaalamu yalikuwa huko na katika nchi za kikomunisti ilikuwa kuongoza inabidi uwe na mamlaka na kudhibiti chama na jeshi na jeshi lipo ndani ya chama.

Hivyo cheo cha Urais China ni kama bosheni tu hakina nguvu kubwa.

2. India
Tuje kwa hili taifa linalo kuja kwa kasi katika uchumi.

India nayo ina cheo cha Urais na Rais wa sasa wa India ni huyu mwanamama anaeitwa Droupadi Murmu licha ya yeye kuwa Rais lakini madaraka makubwa katika nchi ya India yapo chini ya Waziri mkuu wa chama cha BJP bwana Narendra Modi.

Hawa India wanatumia mfumo wa kisiasa unaoshabihiana na Uingereza.

3. Germany
Licha ya kuwa na cheo cha Urais hawa wakoloni wa Tanganyika lakini mamlaka makubwa ya kiutawala Germany yapo chini ya Chancellor.

Hawa wajerumani wanafanana fanana na waingereza.

Chancellor wa sasa wa Germany ni bwana Olaf Scholz.

4. Vietnam
Kama ilivyo kaka yake mkubwa China.

Nchi hizi za kikomunisti madaraka makubwa ya uongozi yanaanzia chamani na cheo cha Urais Vietnam ni kama bosheni tu.

Kiongozi mkuu wa sasa wa Vietnam ni Katibu mkuu wa chama cha kikomunisti cha Vietnam bwana Nguyen Phu Trong licha ya kwamba sio Rais wa Vietnam.

5. Iran
Hii Jamhuri ya kiislam ya Iran nayo kama mataifa niliyotaja hapo juu ya vyeo vya Urais lakini mamlaka makubwa ya uongozi hayapo kwa hao Marais.

Mamlaka makubwa ya uongozi Iran yapo chini ya kiongozi wa kidini kwa kuwa hii ni Jamhuri rasmi ya kiislam.

Na kiongozi mkuu wa sasa wa Iran ni Ayatollah Khomeini.
 
Back
Top