Advertise here

China Yazindua Intaneti Yenye Kasi Kubwa ya 10G

Kasomi

JT Founder
1763634153691 (1).jpg

China imeingia kwenye hatua mpya ya ushindani wa kiteknolojia baada ya kuzindua mtandao wa kwanza wa kibiashara wenye kasi ya 10G (10,000 Mbps) moja kwa moja hadi majumbani. Hii ni hatua ambayo inabadilisha kabisa maana ya “intaneti ya kasi”, kwani faili la filamu ya 4K lenye ukubwa wa GB 20 ambalo lingechukua saa kadhaa kwenye intaneti ya kawaida, sasa linapakuliwa ndani ya sekunde chache tu.

Mradi huu umeanza kutekelezwa katika mji wa kisasa wa Xiong’an, ambapo majaribio ya kwanza yameeonyesha kasi ya karibu 9.8 Gbps, na latency ndogo sana jambo linalowezesha cloud gaming, 8K streaming, huduma za AI kwa wakati halisi, na mifumo ya 'smart cities' kufanya kazi bila kusuasua.

Wakati Marekani bado wastani wa intaneti ya majumbani uko kwenye “kasi ya kawaida”, watumiaji wengi nchini China wanapata fiber ya kasi kubwa kwa bei ya chini takribani dola 15 kwa mwezi ikilinganishwa na zaidi ya dola 75 nchini Marekani. Hii inaifanya China kuboresha miji mizima kwa 10G kama mkakati wa maendeleo, si tu kuboresha burudani.

Ukweli ni kwamba, mataifa yatakayokuwa na miundombinu ya intaneti ya mwendo wa juu zaidi kama 10G ndiyo yatakayoamua wapi utajiri wa kidigitali wa miaka ijayo utaundwa. Kasi ya intaneti inabadilika kuwa sawa na reli, barabara na umeme wa karne ya 21: mwenye spidi ndiye atakayemiliki mustakabali wa teknolojia, biashara, na ubunifu.
 
Back
Top