Simulizi
Member
Anaandika Mdau,
TBT
MASOMO yangu ya Chuo Kikuu niliyasoma kimachale sana! Sikuwahi kukaa hostel za wanafunzi labda kipindi cha mitihani au nilipopigwa sup (supplimentary). Nilihakikisha sidisco lakini ukweli kabisa sikuwa na morali ya kusoma kama ambavyo nilikuwa nasoma nikiwa kidato cha 1 hadi cha 6. Nikashuka ufaulu kutoka mwanafunzi kipanga wa Daraja A hadi kuwa mwanafunzi wa wastani au Daraja B.
Niliingia Chuo Kikuu nikiwa tayari nimeijua pesa kuliko pengine wanafunzi wenzangu wengi na hata baadhi ya walimu wangu. Nilikuwa tayari nimeishajua kusoma na kuandika pesa!
Chuoni niliishi kama digi digi ! Maisha yangu mengi niliyatumia mtaani kuanzia Kigamboni, Magomeni,Kimara hadi Mbezi ! Nikawa naitembea mitaa ya Kariakoo kama mwendawazimu! Nilijifunza somo la "UTHUBUTU" kuanzia hapo.
Acha nikusimulie maisha yangu halisi niliyoishi wakati nikiwa mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya udaktari wa binadamu katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi -Muhimbili kuanzia mwaka 2007 hadi Disemba 2012
Nilimaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2005 ila nikakaa Mtaani miaka 2 kwa KUPENDA mwenyewe. Kipindi chote hiki cha miaka 2 mtaani niliishi Kigamboni - Dar es salaam. Nikawa mwalimu mashuhuri wa kufundisha watu wazima majumbani! Sitasahau kisa kimoja ambacho nilikutana nacho kwenye moja ya nyumba ya wateja wangu usiku nilipoenda kufundisha somo la English kwa mama wa makamo; nikiendesha baiskeli yangu ya gia (Hii naiacha leo
). Sitasahau 

Pia nilikuwa na vituo mbalimbali vya MASOMO ya ziada (Tuition centers). Hadi kesho kuna watu WENGI nikikutana nao wananiita "tiiiichaaaa"
. Kipindi hicho nilifundusha Kila somo kuanzia English , hesabu hadi Historia!! Kila somo Wallah
. Kumbuka sikuwahi kusomea ualimu ! INAKUWAJE wewe mwalimu unashindwa kufanya kama nilivyofanya mimi miaka hiyo??
Mwaka 2007 ndio nikafanya mtihani rasmi wa "Matriculation" UDSM kipindi hicho kabla ya kujiunga kwenye MASOMO ya Shahada ya Kwanza ya udaktari katika Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi -Muhimbili. Kipindi hicho Muhimbili ilikuwa sehemu ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM). Mtihani wa Matriculation ulikuwa ni mtihani wa kupima kama kweli unafaa kujiunga na Chuo Kikuu! Ulikuwa mtihani mwepesi wenye kuchagua YES au NO! Sidhani kama kuna mtu alifeli mtihani huo wa Matriculation! Sidhani!
Tangu siku ya kwanza darasani nilisoma kimachale. Sikuwahi kukaa hostel. Sikuwa maarufu chuoni. Nilikuwa maarufu sana Mtaani. Muda wote nikiwa darasani akili yangu ilikuwa Mtaani; ufaulu wangu ulishuka ila sikufeli. Nilipigwa sup kadhaa
na kuziruka mwisho wa siku nikahitimu na wenzangu
.
Nikiwa chuo Kikuu sitasahau siku ambayo wanafunzi wenzangu darasa zima waliangua kicheko baada ya mimi kuchomoka nduki darasani mara tu baada ya mwalimu kumaliza kipindi. Nikachomoka darasani nikiwa nimevalia helmet na jaketi kubwa (pengine hiki ndicho kilichowachekesha sana wanafunzi wenzangu). Niliendesha pikipiki yangu kisha nikatokomea Mtaani kuwahi deal za biashara hadi siku ambayo wanafunzi wenzangu walinijulisha kuwa kuna test!
.
Nilikuwa mwanafunzi wa "hovyo" sana hasa kwenye mahudhurio ! Ingekuwa kipindi cha shule ya Msingi ningelambwa fimbo kila siku kwa utoro. Nilikuwa mtoro kiasi kwamba hata wanafunzi wenzangu wengi sikuwajua kwa majina wala sura zao
!!
Kipindi nasoma nilikuwa tayari nimeishachungulia Mtaani na kuyajua maisha halisi ya Mtaani. Hii ilinifanya niachane na kauli za mama yangu mzazi za -"Soma mwanangu ufaulu vizuri ili upate ajira ya mshahara mkubwa". Nilikuwa tayari nimeishagundua kuwa haya maneno huenda yalikuwa ya kweli zamani ila sasa yamepitwa na wakati. Nilikuwa tayari nimeishaelewa kuwa -"hakuna kitu kinaitwa mshahara mkubwa".
Nilipevuka mapema! Nilistukia mchezo mapema. Nakumbuka nikinunua gari ya kutembelea kwa mara ya kwanza nikiwa Chuoni mwaka wa 4. Nilikuwa tayari nimeishachungulia Mtaani. Na kwa sasa nimekomaa kupitia Misukosuko na ndio maana nimeanzisha Chuo Kikuu Cha Mtaani -Kitivo Cha Misukosuko ambapo Mimi Mwenyewe ni mhadhiri (lecturer) katika chuo hiki ambacho nakiendesha kupitia group ya WhatsApp. Mwalimu mzuri ni UZOEFU!
Nikiwa mwanafunzi nilikuwa tayari nimeishaonja chungu na tamu za UJASIRI-wA-MALI l. Hamasa yangu ya kusoma ilishuka. Kuna wenzangu WENGI waliodisco (kuachishwa masomo kwa kufeli).
Leo hii naelewa kwa nini baadhi ya watu mashuhuri duniani waliacha masomo vyuo vikuu (drop out). Ni kama walijitafuta na kujipata na kuhisi tena digrii haina maana tena kwenye maisha yao. Sikuwa kama wao; mimi nilikomaa na kumaliza kwa wakati. Kuna waliosomo udaktari huu huu kwa miaka 7 badala ya 5 chuoni!
===
Kama una stori Yako unaweza Andika kwenye jukwaa hili au unaweza tutumia ili kuiandika kwa niaba