Kasomi
JT Founder
KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2026/2027
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linautaarifu umma kuwa Udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2026/2027 kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa na NACTVET umefunguliwa rasmi leo tarehe 28 Mei, 2026.
Maombi ya udahili kwa kozi za Afya na Sayansi Shirikishi -Tanzania Bara, yatafanyika kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (Central Admission System CAS) unaopatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz) kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 10 Julai, 2026 kwa awamu ya kwanza.
Aidha, maombi ya kozi zisizo za Afya na Sayansi Shirikishi, na kozi za Afya na Sayansi Shirikishi zitolewazo katika vyuo vilivyoko Zanzibar yatumwe moja kwa moja kwenye vyuo husika kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 10 Julai, 2026 kwa awamu ya kwanza.
Baraza pia linautaarifu umma kuwa orodha ya kozi zote na vyuo vinavyotoa kozi hizo, inapatikana katika Kitabu cha Mwongozo wa Udahili kwa Mwaka wa Masomo 2026/2027 (Admission Guidebook for Academic Year 2026/2027). kinachopatikana katika tovuti ya Baraza (www.nactvet.go.tz).
Baraza linasisitiza kila mwombaji kuhusika mwenyewe katika zoezi zima la kuomba kudahiliwa, kuandika taarifa zake kwa usahihi na umakini, na kutunza kumbukumbu atakazopatiwa na Baraza kupitia namba yake ya simu, bila kumpatia mtu mwingine yeyote ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika zoezi zima la maombi ya kujiunga na kozi katika vyuo mbalimbali.