Advertise here

Ujio wa simu umeharibu manjonjo na utamu wa kutongoza.

Mtata

Member
Ujio wa simu umeharibu manjonjo na utamu wa kutongoza.

Sio siri ujio wa simu ya kiganja umepunguza majonjo ya kutongoza.

Siku hizi vijana wa kileo hawapati matatizo kama kupigwa na kakamtu, baba MTU au Dada mtu, zamani ilikuwa ni lazima udunde na mwiko au umwagiwa maji wakati unavizia, mbu walituuma sana, makaka walikuwa maadui wa kwanza ukiwa mawindoni. Msichana akianza kukua anaongezewa ulinzi, hata akitumwa chunzi ni lazima aambatane na kitoto kinachojifunza umbeya hasa miaka 7
Siku hizi darasa la nne naye anasimu na anatafuta boyfriend na kumwonyesha mama, wakati mwingine wakati wa siku ya kuzaliwa kwake anamlazimisha mama kuwa ni lazima awepo.

Vijana mmepoteza uwezo na manjonjo ya utunzi wa maneno matamu yenye ushawishi wa hali ya juu kumvutia msichana naye akapata raha jinsi unavyompanga na kumpamba.
Yaani siku hizi mnatongoza hivi;
Dada vipi
Safi
Samahani naomba no. Yako
Akishatoa anapiga pale pale kuakiki, utasikia nilizani umenipa no ya Gari; poa basi nitakucall
Baada ya nusu saa ashatoka ATM utasikia UKo wapi tukapate juisi. Hapo kamaliza mchezo.
Tusiendeleze uonevu huu wa kukwepa kutongoza kwani mnamwondolea raha mtongozwaji anashindwa kulemba macho, kujinyonga nyonga mikono, kungata kidole kutafuna kucha , kuandikia kidole cha mguu ardhini kulalisha shingo kwa maringo huku mmm mmm zikiwa nyingi na hapana kibao.
Huu ni uonevu kutomvizia vizia Mara kwa Mara kuonyesha juhudi za kumhitaji. Sio anamaliza juice unaota tex mwende baa yenye guest
 

Similar threads

Back
Top