Kasomi
JT Founder
Kabla ya michezo ya kisasa ya Android na iOS kuwa ya kawaida, kampuni ya Gameloft ilikuwa moja ya majina makubwa zaidi kwenye soko la michezo ya simu miaka ya 2000 hadi mapema 2010.
Enzi za simu za Java (keypad phones) na zile za mwanzo zenye touchscreen, Gameloft ilishangaza wengi kwa kutoa michezo yenye ubora wa juu licha ya uwezo mdogo wa vifaa hivyo. Walifanikiwa kuleta graphics nzuri, hadithi za kuvutia na gameplay iliyokuwa karibu na ile ya console kitu ambacho hakikuwa cha kawaida wakati huo.
Baadhi ya michezo yao iliyotikisa sana ni kama:
Asphalt 5
Modern Combat: Sandstorm
Nova
Prince of Persia Classic
Kwa wengi waliokua na simu za Nokia, Sony Ericsson au Samsung za zamani, Gameloft ilikuwa sawa na “console ndani ya mfuko.”
Kadri teknolojia ilivyokua na kampuni nyingine kuingia sokoni kwa nguvu, ushindani uliongezeka, lakini mchango wa Gameloft katika kuendeleza mobile gaming hauwezi kupuuzwa.
Wewe ulikuwa unacheza game gani ya Gameloft enzi hizo?