Kasomi
JT Founder
Kila ifikapo Januari 07 kwa kila mwaka huwa pia ni sikuku ya Krismasi, Wakristo wa madhehebu ya Orthodox husherehekea kuzaliwa Yesu Kristo kila Januari 07 tofauti na madhehebu mengine mengi duniani ambayo Krismasi huwa Disemba 25.
Sababu kubwa ni kwamba Kanisa la Orthodox linafuata kalenda ya kale ijulikanayo kama Kalenda ya Julian tofauti na Kalenda ya Gregory inayotumiwa kwa sehemu kubwa ya dunia.
Kanisa la Orthodox lina waumini wapatao milioni 300 kote duniani. Wengi wanapatikana Ulaya Mashariki, Ugiriki, Ethiopia na maeneo kadhaa ya Mashariki ya Kati.