Advertise here

TANZIA Prof. Honest Ngowi afariki Dunia

Kasomi

JT Founder
222334444-1-660x400.jpg

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka ametangaza kifo cha Prof. Honest Ngowi na Dereva wake, waliofariki asubuhi ya leo kwa ajali ya gari wakiwa njiani kwenda Kampasi Kuu Morogoro.

MPYAAAA-360x220.jpg

"Tunaomba muwe watulivu wakati Menejiementi inaendelea kufuatilia taarifa kamili ya tukio hili, na kuweka taratibu zingine, taarifa zaidi zitatolewa rasmi na taratibu zingine za kuwahifadhi wenzetu, Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina la Bwana lihimidiwe. Poleni Wote kwa msiba huu mzito“
-Ofisi ya Mawasiliano Mzumbe.


=======

Professor Honest Prosper Ngowi (PhD Economics) alikuwa mkuu wa idara ya kozi fupi, utafiti na ushauri chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya ushauri ya ANO. Katika maisha yake amekuwa mtafiti, mshauri na kuchapisha machapisho ya kitaaluma zaidi ya 60, tafiti zaidi ya 70 pia makala zaidi ya 250 kwenye magazeti.

Prof. Ngowi amebobea kwenye uchumi wa maendeleo na biashara hasa kwenye uchumi mkubwa, biashara ya kimataifa, uwekezaji wa kigeni, ujasiriamali, uchumi wa mafuta na gesi na mengineyo. Prof. Ngowi pia amefanya kazi kama msahihishaji wa nje kwenye vyuo mbalimbali ikiwemo chuo kikuu cha Makerere, Udsm, North West University(Afrika kusini) na vingine vingi.
 
Last edited:
Back
Top