Kasomi
JT Founder
Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana imeandaa Shindano la Vijana Uchumi Challenge lenye kauli mbiu ‘Wana tunafikiri, Taifa linasonga’.
Shindano hili linalenga kukuza Mawazo ya vijana, yenye ubunifu, yanayotekelezeka na endelevu katika kulinda na Kukuza Uchumi wa Taifa letu dhidi ya athari za misukosuko ya kimataifa.
Swali muhimu katika shindano hili ni;
“Inapotokea tishio la Uchumi wa Dunia kushuka kutokana na misukosuko ya kimataifa ikiwemo vita, ushindani wa kiuchumi na kiteknolojia, ni changamoto zipi zinazoweza kuikumba Tanzania; na nini kifanyike ili uchumi wa Tanzania uendelee kuimarika?”
Shindano hili linakaribisha ushiriki wa kijana yeyote wa kitanzania mwenye umri kati ya miaka 15 – 35.
Ili kushiriki, kijana mmoja mmoja anakaribishwa kuwasilisha wazo lake, kwa njia ya maandishi yasiyozidi maneno 300 au kwa njia ya video isiyozidi dakika 3 kupitia kiunganishi: hiki hapa chini
Kabla ya Tarehe 30 April 2026. Wazo linalowasilishwa ni sharti likidhi vigezo vifuatavyo ambavyo vitatumika kupata washindi:
1. Ubunifu: Kiwango cha fikra mpya na upekee wa wazo.
2. Uelewa wa Changamoto za Kiuchumi: Kiwango cha uelewa wa mshiriki kuhusu changamoto za kiuchumi za sasa na muktadha wa kimataifa.
3. Uhalisia: Utekelezekaji wa wazo na uwezekano wake kutekelezwa kwa vitendo.
4. Athari kwa Uchumi: Mchango unaotarajiwa wa wazo katika kukuza uchumi wa taifa.
5. Uwezo wa Kuleta fursa: Uwezo wa wazo kuzalisha na kuongeza fursa za ajira kwa vijana
6. Uendelevu: Uwezo wa wazo kudumu na kuleta matokeo chanya ya muda mrefu.
7. Ubora wa Uwasilishaji: Mpangilio, uwazi na urahisi wa kuelewa pendekezo.
Vijana Wote Mnakaribishwa.

Bonyeza hapa