john achila mukumwa
Member
Yesu aliwezaje kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa
Wakati shetani anamjaribu Yesu, biblia inasema alimchukua na kumpandisha kwenye kinara cha hekalu. Swali ni je! alikuwa anachukuliwaje mahali pale, ni njia gani ilikuwa inatumika?
Ni muhimu kufahamu kuwa Bwana Yesu hakupelekwa sehemu nyingine yo yote ili kujaribiwa zaidi ya pale jangwani. Hii ikiwa na maana kuwa majaribu yake yote yalimtokea akiwa pale pale jangwani.
Tuangalie kitabu cha Mathayo 4:
1 “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi,
2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa”.
Swali: kama ni hivyo iweje, shetani amtoe pale na kumpeleka kwenye kinara cha hekalu, na wakati huo huo amwoneshe milki zote za ulimwenguni? Je, aliondokaje pale? au alichukuliwa kimazingara?
Kitabu cha Mathayo 4 kinaendelea kusema:
5 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. 10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. 11 Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia”.
Maelezo ni kwamba, majaribu yale yalikuwa katika roho, na siyo katika mwili.
Kwa ufupi, yalikuwa ni mfano wa maono. Kikawaida, maono yanaweza kuja ikiwa ni ya kukuonesha tukio husika. Utashangaa unaweza kujiona kama upo pale pale eneo lenyewe, lakini kumbe sivyo.
Inakuwa kama ndoto tu. Unaota upo kijijini kwenu, unashughulika, unaongea na ndugu, lakini kiuhalisia wala hujasafiri, bali kumbe umelala pale pale kitandani kwako. Ni katika ukimwengu wa roho.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu. Alikuwa pale pale jangwani, wala hakutoka. Isipokuwa alikuwa katika roho, akayaona hayo yote, aliyooneshwa na shetani.
Kwa hiyo, Yesu alikuwa pale pale jangwani. Lakini, alikuwa anapambana na shetani katika ulimwengu wa roho, akiwa pale pale, bila kusafiri kimwili.
Yesu kuchukuliwa na shetani juu ya kinara cha hekalu kujaribiwa, ilikuwa ni kiroho, na siyo kusafiri kimwili. Njia iliyokuwa ikitumika ni ya kiroho.
Tukumbuke kuwa shetani ni roho, hana mwili. Hivyo, Yesu alipambana naye na kumkemea katika ulimwengu wa roho.