john achila mukumwa
Member
Yesu Alipopanda Mlimani Kuomba kwa Nini Alitokewa na Musa na Eliya?
Katika ule mlima mrefu, aliopanda Yesu na wanafunzi wake kuomba, kwa nini atokewe na Musa na Eliya na siyo manabii wengine, kama vile Isaya au Samweli? au Ezekieli?
Kutokewa na wale watu halikuwa kwa lengo lake. Bali lilikuwa kwa lengo la wale wanafunzi aliokuwa nao, ili kutimiza malengo kadhaa.
Malengo hayo yametajwa hapo chini.
1. KUTIMIZA UNABII MKUU ULIOMHUSU YEYE
(a) Unabii wa kwanza ni ule alioutoa Musa kuwa atakuja Nabii mwingine kama yeye na kwamba watu wamsikilize.
Kumb la Torati 18:15; Matendo 3:22-25:
"BWANA, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye".
Hivyo, Wayahudi walikuwa na matarajio ya kuona mtu anayefanana na Musa, atakayeleta sheria mpya, akija duniani, lakini akiwa na nguvu na uweza mwingi mfano wa Musa.
Ndiyo sababu ya Musa kutokea mbele ya wanafunzi wake, ili Mungu awathibitishie kuwa huyu ndiye yule Musa aliyemnenea habari zake.
(b) Unabii uliohusu kutangulia kwa Eliya kabla ya kuja kwake duniani.
Wanafunzi walikuwa na dukuduku kama huyu ndiye Kristo aliyetabiriwa au siye, na kama ndiye, mbona Eliya hajatangulia mbele yake tukamwona? Kwa sababu waliambiwa hivyo na waandishi. Lakini walipomwona Eliya mwenyewe amesimama mbele ya Yesu wakaamini, lakini bado hawakuelewa.
Walipokuwa wanashuka, ndiyo wakapata nguvu ya kumuuliza Yesu hilo swali.
Na hili ndilo lilikuwa jibu lake, kupitia Mathayo 17:9-13:
9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwaagiza, akasema, Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.
10 Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, Basi kwa nini waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
11 Naye akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote,
12 ila nawaambia, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
13 Ndipo wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
2. KUONDOA UTATA KUWA YEYE SIYO MMOJAWAPO WA MANABII WAKUBWA WA KALE WANAODHANIWA
Utakumbuka kabla ya kupanda mlimani aliwauliza: watu wanamzungumzia kuwa yeye ni nani? Wanafunzi wakamjibu kuwa wanasema yeye ni Eliya, Yohana Mbatizaji, Yeremia, wengine mmojawapo wa manabii wa kale (Mathayo 16:13-18).
Hivyo kulikuwa na utata mwingi. Lakini siku hiyo aliondoa utata huo.
Mitume walipoona sura za manabii wao wa kale wamesimama mbele ya Yesu, mwenye utukufu mwingi sana kupitia wao, wakaamini kuwa yeye ni zaidi ya manabii wote wakubwa kwa wadogo, waliowahi kutokea katika historia.
3. KUWAFUNULIA KUWA ATAKUFA KAMA MMOJAWAPO WA MANABII WAKUBWA, LAKINI PIA ATAPAA KAMA MMOJAWAPO WA MANABII WAKUBWA
Musa alikufa, lakini Eliya alipaa.
Yesu ndiye mtu pekee miongoni mwa wanadamu, aliyekufa, kisha akazikwa, kisha akafufuka, na mwisho akapaa.
Kwa hiyo, ile ilikuwa ni lugha ya kinabii, kueleza hatma yake, na ndiyo maana hata manabii hao walikuwa wakizungumza mambo yahusuyo kufa na kufufuka kwake (Luka 9:31).
Hizo ndizo zilikuwa sababu kuu za Bwana, kwa nini alitokewa na Musa na Eliya na siyo manabii wengine tofauti.
Walipokuwa wanashuka, Yesu akawaambia wanafunzi wake wasimwambie mtu hadi atakapofufuka katika wafu.
Siyo wote watamwona Yesu katika kilele cha utukufu wake, isipokuwa wale tu walio na kiu na yeye. Ambao watakuwa tayari kuwa karibu naye wakati wote, mfano wa hao wanafunzi watatu yaani Yohana, Petro na Yakobo.
Ukimpenda Yesu tumia muda mwingi kuwepo uweponi mwake. Utamjua sana kwa mapana na marefu yake. Utamjua sana kwa kusoma Neno la Mungu, yaani Biblia.