john achila mukumwa
Member
Kwa Nini Yesu Aliwaambia Baadhi ya Aliowaponya Waende Kujionyesha kwa Makuhani
Kuhani ni nani
Kuhani ni mtu ambaye katika dini nyingi, anashika nafasi ya mshenga kati ya Mungu na binadamu.
Kitabu cha Waebrania 3:7-8: "Ikiwa leo mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu." Waebrania 7:17 “Wewe ni kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeki. Waebrania 8:3 “Basi kila kuhani mkuu huwekwa ili kutoa matoleo na dhabihu”.
Makuhani wa Mungu katika biblia ni watu waliotiwa mafuta na kuteuliwa na Mungu kwa kazi zote za ibada mbele za Mungu kwa ajili ya watu wake. Kwa mfano; upatanisho wa dhambi, na watu hawa ndio wana nafasi au uwezo wa kumsogelea Mungu kwa ukaribu zaidi.
Neno Kuhani katika Agano Jipya lina maana mtoto wa mfalme au mtumishi. Makuhani wote kwenye maandiko ni lazima wawe na madhabahu na ni lazima watoe sadaka.
Baada ya kuwaponya watu, Yesu aliwaambia waende kujionyesha kwa makuhani
Kwa nini Bwana Yesu aliwaambia wale watu wenye ukoma, waende kujionyesha kwa makuhani? Kwa nini asiwaponye tu hivyo hivyo na kuwaacha, mpaka awaambie waende kwa makuhani.
Luka 17:12 “Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,13 wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! 14 Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika”.
Tujue kuwa Injili ya Kristo inawafikia watu katika namna mbili, wengine kwa kuwaokoa, na wengine kama ushuhuda kwa watu (Mathayo 24:14).
Kuhusu uponyaji wa Yesu pia ni hivyo hivyo. Alikusudia uwafikie watu kwa namna mbili. Moja ni kuokoa, na pili ni kuwa ushuhuda. Si kila uponyaji au muujiza Yesu aliokuwa anaufanya ulikuwa ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Hapana. Ponyaji nyingine aliziruhusu mahsusi kwa lengo la kuwa ushuhuda kwa wengine, ili siku ile ya hukumu wasije wakasema hatukuona, au hatukusikia.
Tunasoma jambo kama hilo katika Mathayo 8:1 “Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. 2 Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. 3 Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika. 4 Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao”.
Hicho kitu ndicho kilichowakuta makuhani, mafarisayo na waandishi. Ni watu ambao walikuwa hawataki kusikia wala kuamini.
Hivyo, Bwana Yesu, alipowaponya baadhi ya watu, hakuwaacha tu hivi hivi waende, kama alivyofanya sehemu nyingine, bali aliwaagiza waende kuwaeleza makuhani miujiza iliyowakuta.
Kwa hiyo, walikuwa wanapokea shuhuda nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali walioponywa. Pengine kwa siku hata watu 100. Na kila walipoulizwa ni nani kawaponya, wanamtaja Yesu.
Hivyo hata sisi, tusifurahie tu miujiza. Mungu anatuletea miujiza mingi, watu wanaponywa, wanafunguliwa, na huku wengine maisha yetu yapo nje ya Kristo. Tusifurahie kwa sababu tujue kuwa hiyo ni hukumu tunajiandikia. Na ndiyo maana Bwana alisema maneno haya sehemu fulani:
Mathayo 11:21 “Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. 22 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. 23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo. 24 Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe”.
Hivyo, hiyo ndiyo iliyokuwa sababu kwa nini Yesu aliwaambia wakajionyeshe kwa makuhani. Ni kwa sababu wao ndio walikuwa hawamwamini wala kuziamini kazi zake.
Lengo la Yesu kuwaambia baadhi ya aliowaponya kwenda kujionesha kwa makuhani, lilikuwa ni kupeleka ushuhuda (sawa na kupeleka salamu) kwa makuhani hao, ili waamini, kwa sababu walikuwa wabishi kuamini uponyaji uliokuwa ukifanywa na Yesu.