john achila mukumwa
Member
Je wakati Yesu anazaliwa shetani alikuwa amefungwa?
Kulingana na Mathayo 12:29, je, Yesu alikuwa amemfunga shetani wakati wa kuzaliwa kwake?
Ili kupata jibu, ni vizuri turejee Mathayo 12:29:
“Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
1. Hivyo, jibu ni kwamba shetani hakuwa amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana Yesu. Na hata sasa shetani hajafungwa, kwani ingekuwa shetani amefungwa wakati wa kuzaliwa Bwana, basi Herode asingetafuta kumwua mtoto; kwa maana shetani alikuwa huru na alitaka kumtumia Herode kumuangamiza Yesu.
Pia, Mathayo 2:13 inasema: “Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize”.
Mathayo 4:1 “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.
2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa. 3 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate”.
3. Aidha, ikiwa shetani amefungwa, leo maasi yasingeendelea kuwepo na maandiko yasingetuonya kuwa tusimpe nafasi:
Waefeso 4: 27 “wala msimpe Ibilisi nafasi. 28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji”.
Je, Shetani atafungwa lini
Maandiko yametabiri shetani kuja kufungwa katika ule utawala wa miaka elfu wa Bwana wetu Yesu hapa duniani. Na utawala huo utaanza baada ya dhiki kuu kuisha, na hukumu ya Mungu kwa mataifa kupita (Ufunuo 16). Hapo ndipo utawala wa miaka elfu moja utakapoanza na shetani (pamoja na majeshi yake) kufungwa kwa kipindi hiko.
Kitabu cha Ufunuo 20:1 kinasema: “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache”.
Maana ya maandiko katika Mathayo 12:29 ni nini
Turejee andiko hilo:
29 “Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, Asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
Hayo ni maneno ambayo Bwana Yesu aliyasema, akifundisha nguvu iliyo KUU (kubwa) inapoingia mahali, basi INATEKA AU INAFUNGA ILE NGUVU ILIYO DHAIFU.
Ukisoma kuanzia juu kidogo utaona ni wakati ambapo Mafarisayo walimwona akitoa pepo kwa uweza wa Mungu, lakini wakasema yeye hatoi kwa uweza wa Mungu bali kwa uwezo wa Pepo mkuu aitwaye Beelzebuli, ambaye ni shetani mwenyewe.
Na Bwana akawahoji, akiwauliza: yawezekanaje Shetani amtoe shetani mwenzake? Ni jambo ambalo haliwezekani. Vinginevyo ufalme wa giza hauwezi kusimama. Lakini kama wakiona pepo ametolewa, maana yake ametolewa kwa uweza wa Mungu, kwa sababu kamwe shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake.
Ili kulifanya hilo lizidi kueleweka vizuri, ndiyo maana Yesu akatoa mfano mwingine kwamba: “Awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
Hii inafunua kuwa Bwana anapotoa pepo, kwanza anauteka ule ufalme wa giza (maana yake ufalme wote unakuwa chini ya amri yake), halafu ndipo anaamrisha pepo zitoke na kwenda atakako yeye (Mathayo 8:28-32).
Kitendo cha Bwana Yesu kusimama na kuamrisha, maana yake mamlaka yake ni KUU inayoteka, na kufunga, na kuhamisha. Na mamlaka hiyo haijabaki kwake tu peke yake, bali pia amewapa na wale wote wanaomwamini na kufanya mapenzi yake, kwamba kwa jina lake wanateka, na wanafunga na kuhamisha kila falme za giza:
2Wakorintho 10 inasema: 4 “maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia”.
Mantiki ya Bwana Yesu hapo ya kufunga, haikuwa ya kumfunga shetani asiwepo duniani, bali katika kuzifunga kazi za ibilisi na majeshi yake zisisimame mbele yetu. Lakini, shetani yupo, na ataendelea kuwepo na kuwasumbua wale wote wasiomwamini na kumfuata Bwana Yesu, lakini walio na Bwana shetani hana nguvu juu yao.
Kwa hiyo, wakati Yesu anazaliwa, shetani alikuwepo, na hakuwahi kufungwa wakati wo wote huko nyuma, yupo hata sasa, lakini atakuja kufungwa baada ya hukumu ya Mungu kwa mataifa, kama inayotajwa katika kitabu cha Ufunuo 16.