Matokeo ya Mtihani wa NECTA: Kiwango cha ufaulu cha Darasa la Saba chapanda hadi asilimia 85.22

Kasomi

JT Founder
1000978084.jpg

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) uliofanyika Septemba 2026, yakionesha kuwa watahiniwa 970,876 sawa na asilimia 85.22 wamefaulu.

Akitangaza matokeo hayo Novemba 03, 2026, Katibu Mtendaji (NECTA), Profesa Said Mohamed, ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.42 ikilinganishwa na asilimia 81.80 iliyorekodiwa mwaka 2025.

Kwa kuzingatia jinsi, wasichana 527,622 sawa na asilimia 84.43 wamefaulu, wakati wavulana 443,254 sawa na asilimia 86.18 wamefaulu.

NECTA imeeleza kuwa ufaulu wa wasichana umeongezeka kwa asilimia 3.22 kutoka asilimia 81.21 mwaka 2025, huku wavulana ukiongezeka kwa asilimia 3.67 kutoka asilimia 82.51.

Aidha, watahiniwa 429,667 sawa na asilimia 37.72 wamepata madaraja ya A na B, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.82 ikilinganishwa na mwaka 2025.

Tazama Matokeo hapa​

 
Back
Top