Kasomi
JT Founder
Mahakama Kuu ya Tanzania imemhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kifungo cha miaka minne jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi.
Hukumu hiyo imetolewa leo, Novemba 6, 2026, na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru. Mahakama pia imemweleza kuwa ana haki ya kukata rufaa.
Awali, akizungumza kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Lissu alisisitiza kuwa haombi msamaha kwa sababu anaamini hana hatia. Alipinga kutiwa hatiani kwa uchochezi, akisema shtaka alilokuwa akikabiliwa nalo lilikuwa la uhaini.
Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025, baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma. Baadaye alisafirishwa kwenda Dar es Salaam na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 10, 2025, ambako alisomewa shtaka la uhaini.
Hadi leo, amekuwa kizuizini kwa takribani mwaka mmoja na miezi saba akisubiri kukamilika kwa kesi yake. Akizungumza mahakamani kabla ya kupewa adhabu, Lissu amesema leo ni siku yake ya 577 akiwa mahabusu.
====
Baadhi ya Matukio Mengine ambayo yalitokea kabla ya huku hiyo ni kama ifuatavyo.
1- Lissu Atiwa Hatiani Kosa La Uchochezi
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam, imemtia hatiani Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kwa kosa la uchochezi, baada ya kumuondolea hatia katika shtaka la uhaini lililokuwa likimkabili.
Hukumu hiyo imesomwa leo, Ijumaa, Novemba 6, 2026, na Jaji Dunstan Ndunguru, kiongozi wa jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo.
Mahakama imesema upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha kuwa Lissu alikuwa na nia ya kuitishia Serikali kupitia kauli zake. Hata hivyo, imeridhika kuwa kosa la uchochezi limethibitishwa na kumtia hatiani kwa kosa hilo kama mbadala wa shtaka la uhaini.
Akifafanua uamuzi huo, Jaji Ndunguru amesema Kifungu cha 319 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinaipa mahakama mamlaka ya kumtia mshtakiwa hatiani kwa kosa dogo lililothibitishwa kama mbadala wa kosa kubwa, hata kama hakushtakiwa kwa kosa hilo dogo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyosomwa mahakamani, Lissu ametiwa hatiani kwa kosa la uchochezi chini ya Kifungu cha 390 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
2- Lissu akijitetea kwa kosa alilopewa
"Siku 577 nikiwa gerezani kwa kuitwa Muhaini kosa ambalo kwa katiba ni kosa kubwa kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania''.
''Leo mnaniita mchochezi kwa kosa ambalo halina adhabu yani baada ya kukaa siku 577 kusubiri kitanzi , mmeniita mchochezi na wakili wa serikali mkuu anahangaika kutafuta adhabu yake ni nini''
Hii maana yake ni nini waheshimiwa majaji? Maana yake ni kwamba kosa nililoshtakiwa nalo.halikua kosa"
Ushahidi wangu umethibitisha hii ilikua ni kesi ya kisiasa kugeuza mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa.
Ni political persecution, kwa hiyo inabidi visababu vitengenezwe kumfunga huyu mgomvi wetu wa kisiasa.
Na visababu vyenyewe ni kosa la.uchochezi ambalo mmelitengeneza sikushtakiwa nalo .
Nje ya uhaini nilishtakiwa kusambaza taarifa za uongo na hilo mmesahau.