Advertise here

Kuachwa au kukataliwa na mtu unayempenda ni Moja ya matukio yanayotisha sana Kwa mtu yeyote

Kasomi

JT Founder
Anaandika Emmanuel Minga

Kuachwa au kukataliwa na mtu unayempenda ni Moja ya matukio yanayotisha sana Kwa mtu yeyote.

Huwezi amini kila mtu anahofu ya kuachwa na mtu anayempenda sana.(behavior science prove this)

Maumivu ya kuachwa na mtu uliyempenda siyo mchezo, tusiadanganyane hapa lazima moyo uume na machozi yatoke hata Kwa kulenga lenga bhana huhuuu???? ( nacheka lakini naogopa)

Lakini habari njema ni kwamba unaweza kuikabiri hali hili katika namna Bora ambayo hata yule aliyekuzingua anaweza kujuta kwanini alikupoteza.

Kuna hatua chache nitakupa Leo ....lakini Kwa maelezo deep nitafute nikupe kitabu changu cha usiteseke tena.

1:: Rekebisha mtazamo wako kwanza.
Umeachwa sawa lakini wengi wetu tunachukua hatua isiyo sahihi kutaka mumuonyesha aliyekuacha amekosea na unatamani aharibikiwe.

Usiwe mtu wa hivyo utaishusha thamani yako na huyo mtu ataona alifanya maamuzi sahihi kukuacha.

Unapaswa ujiambie ukweli kwamba yeye aliyekuacha hana lolote na hausiki chochote kwenye maisha yako hivyo kuendelea kumfwatilia maisha yake hakutokuongezea kitu wewe zaidi ya kupoteza muda wako bure.

Sasa unapaswa ugeuze shabaha yako , badala ya kupoteza muda kumfwatilia tumia muda kuwekeza kwenye kujiboresha na kufanya kazi.

Aliyekuacha akiona haumfwatilii utakuwa umemuachia maswali mazito asiyoweza kuyajibu , anaweza kuanza kujiuliza huwenda alifanya makosa kukukataa. Hii itamfanya yeye ndio aanze kuteseka Kwa ajili yako.

2:: kuwa Bora kuliko ulivyokuwa wakati upokuwa naye.
Kipindi hiki jitahidi kuwekeza zaidi kuzalisha fedha , fanya kazi na kula vizuri, Vaa vizuri boredha muonekano wako, hakikisha shavu limetoka na linang'aa Ili ajiulize yeye ndiye alikuwa chazo cha wewe kutokunawili? Huhuu jitahidi kuonekana vizuri utakuwa na mvuto .

Hii itakusaidia Kwasababu hata watu wako wa karibu wataanza kukuzungumzia kwamba umebadilika na huwenda hata yeye akapata taarifa Kwa wale mabest zake wambeya(utani bhana) , hii itamtamanisha kutaka kujua ni kitu gani umekutana nacho kinachokupa furaha na kukufanya uwe vizuri kiasi hicho.

Hapo Wala hujaongea naye na Wala Huna time naye ila anamtesa Kwa muonekano wako.

Hakuna maumivu makali mtu anayopata kama Yale ambayo anayapata anapomshuhudia mtu aliyemuombea aharibikiwe akakuta ndiyo anazidi kufanikiwa duuu ni kero ujue na inakera haswa .

Na hapa usiigize. Yaishi maisha hayo kweli , Ukiwa busy sana utamsahau na hutateseka tena kuhusu yeye isipokuwa mateso yatahamia kwake, huhuu ni mwendo wa kutamba????????

Basi bwana niishie hapo nisimalize utamu wote. Pata kitabu changu cha usiteseke tena

E.M✍️
 

Similar threads

Back
Top