VITA YA MADENI; AINA KUU 2 ZA MADENI

Kasomi

JT Founder
VITA YA MADENI; AINA KUU 2 ZA MADENI.

Anaandika Festo Amos

Wengine madeni yanawaua wengine madeni yanawainua, walio chini yanawadidimiza na walio juu yanawapaisha, wenye hekima hutumia mikopo kama daraja la wajinga hutumia mikopo kama kamba za kunyonga maisha yao.

Lakini yote katika yote ili kuishinda vita ya madeni ni muhimu kufahamu haya mambo mawili..

Kuna aina kuu 2 za madeni.

Aina ya kwanza ni madeni mazuri na aina ya pili ni madeni mabaya.

Soma kwa makini ili kujua unaangukia kwenye aina gani ya madeni.

Madeni mazuri ni yale ambayo marejesho yake hayatokani na chanzo kingine cha mapato bali deni linajilipa lenyewe.

Madeni mabaya ni yale ambayo malipo yake yanatokana na chanzo kingine cha mapato.

Kwa mfano. Umekopa pesa benki na kujenga nyumba, halafu unatarajia kulipa deni hilo kwa kukatwa mshahara wako, hilo deni ni baya.

Kama umekopa pesa ili ulipe ada ya shule, hilo deni ni baya kwa kuwa utalazimika kutumia pesa nyingine kutoka sehemu nyingine ili kuja kulipa deni lako.

Matajiri wengi wana madeni mazuri, kwa sababu wanakopa ili kuzalisha.

Maskini wengi wana madeni mabaya, wanakopa pesa halafu wanaitumia kisha wanaanza kuhangaika kurudisha deni hilo.

Hii husababisha watu kushindwa kusonga mbele kwa kuwa muda mwingi unautumia kulipa deni ambalo pesa yake ulishaitumia pasipo kuizalisha.

Sasa kwa kuwa umeelewa tofauti hizo unaweza kujifanyia tathmini...

Je binafsi uko kundi gani? Na mara nyingi umekuwa ukiishi na madeni mazuri au mabaya?

Ukishajitambua, basi chukua hatua...

Ishinde vita ya madeni, uweze kuishi maisha makubwa yenye amani na furaha.
_________________________
FESTO AMOS
@Coach Amos
Financial Trainer
0766181367.

Mwandishi wa kitabu cha Nguvu ya pesa,na Mwongozo wa nidhamu ya fedha. nawasaidia watu kujenga nidhamu ya fedha kwa vitendo.

Stay dept free
LIVE A GREAT LIFE.
 
Upvote 0
Back
Top