Kasomi
JT Founder
Rais Donald Trump wa Marekani dakika kadhaa zilizopita ameishukuru Iran kwa kile alichokiita “taarifa ya mapema” baada ya Nchi hiyo kushambulia kambi ya Wanahewa ya Marekani iliyopo Nchini Qatar ambapo hata hivyo amesema hakuna Mmarekani hata mmoja aliyejeruhiwa kutokana na makombora hayo ya Iran.
“Hakuna Mmarekani aliyejeruhiwa na hakuna uharibifu wowote uliofanyika katika shambulio la kombora la Iran, iende kwa Amani na Utangamano katika Eneo hilo, na kwa shauku nitahimiza Israel kufanya hivyo, ninataka kuishukuru Iran kwa kutupa taarifa ya mapema ambayo imesababisha kisitokee kifo chochote, hakuna Mtu aliyejeruhiwa” ——— Trump.
Hiyo ni sehemu ya maneno aliyoyaandika Rais Donald Trump katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social ambapo pia alimshukuru Kiongozi Emir wa Qatar kwa yote ambayo amefanya katika kutafuta amani katika ukanda huo na kuongeza pia maneno yafuatayo “HONGERA ULIMWENGU, NI WAKATI WA AMANI”
Wizara ya Ulinzi ya Taifa la Qatar imesema iliyanasa na kuyadungulia baharini makombora 11 kati ya 12 yaliyorushwa na Iran kuilenga kambi ya anga ya AI Udeid inayoendeshwa na Marekani ambapo kombora pekee ambalo halikudunguliwa, liliangukia katika kambi hiyo lakini halikusababisha hasara yoyote.
Chanzo: MillardAyo UPDATES