Advertise here

UZI WA KIJOBLESS NA MBINU ZA KIDIGREEE

Mtata

Member
Miaka ya nyuma kidogo, nilikuwa na date na mdada mmoja hivi. Huyu mdada tumuite Adola.
(sio jina lake halisi)

Huyu Adola alikuwa na rafiki yake mmoja mzuri sana, yule rafiki yake alikuwa na sifa za Wife material ninaemtaka. Kiufupi rafiki wa Adola ndio alikuwa mwanamke wa ndoto zangu.

Baada ya kumuona rafiki yake Adola ndio nikakumbuka ule msemo wa kabla hujamtongoza hakikisha unawajua marafiki zake wote 🥲.
Huyu rafiki yake tumuite Purity
(Sio jina lake halisi)

Basi kipindi mimi nadate na Adola alikuwa anapenda sana kumuongelea Purity na mara nyingine kuja nae mpaka nyumbani kabisa
(Ile niliyokuwa nakaa ni nyumba sio geto, maana ilikuwa na sifa za kuitwa nyumba. Ghetto wanakaa wakina @Kunguru wa Manzese @Ramadhani majidi nasoro @Rafiki9117 na @maextro na wewe hapo unaesoma nyie ndio mnakaa magetoni)

Siku moja nikachukua namba ya Adola ili nichukue namba ya future wife wangu Purity.

Kwanza Adola hakuwahi kunivutia kivile, basi tu wakati namfuata ni kama kila msichana aliamua kunikataa, nikasema nitadate na chochote ilimradi linapumua. Hicho chochote ndio Adola sasa.

Dakika, masaa, siku hatimaye miezi ikapita, namba ya Purity ninayo sijawahi futa. Kama bahati hivi Adola akawa ameondoka ameenda dar jiji la kitapeli.

Kufika dar akaanza kujikuta matawi sana mimi sio level zake, basi tukawa tumeachana, ikawa ni muda wa kwenda kwa Purity.

Remember Purity anajua kuwa natoka na rafiki yake Adola, maana hata kwenye simu kila mmoja alimsave mwenzake TWINIE. ila matwinie haya bhana.....

Purity namba yake ninayo na sijawahi mtafuta, nitaanzaje kumtafuta na akisema namba nimeipata wapi itakuwaje. Basi hapo nikaja na mpango kabambe ili isiwe ngumu kuingia kwenye maisha ya Purity

Kuna huyo rafiki yangu mmoja, yeye tumuita Josh.

Josh alikuwa ni mwanangu sana hajawahi kunisnich hata mara moja, alikuwa mwana mwana kweli.

Nikamfuata, nikamwambia kila kitu kuhusu huyo Adola na Purity.

Mpango ulikuwa hivi, mimi nitampa namba ya Purity ili achat naye na wakutane kama marafiki wakianza kuzoeana Josh aje anitambulishe mimi kwa Purity ndio nichukue namba. (Sijui kama mnaelewa nyie majamaa mmevurugwa na ada za januari)

Basi kweli mpango ukaenda kama ilivyokuwa bhana wakakutana, wakafahamiana wakawa marafiki, basi siku moja Josh akamleta Purity nyumbani.

Ikawa like

Josh:purity meet my friend CRARENCY

Purity: wooooa waoooo kumbe ni huyu namjua ni shemeji yangu

Mimi kimoyomoyo (shemeji which, shemeji where who is your shemeji )

Basi siku hiyo ndio nikachukua namba ya Purity. Kwanza tukubaliane hapa mpango wa kuchukua namba ya Purity ulifanikiwa kwa asilimia 100. Chukua mbinu hiyo.

Basi wakati nachat na Purity alikuwa anapenda sana kuniita shem shem jina nilikuwa silipendi hilo, siku moja ikabidi nimwambie ukweli kuwa tulishabwagana na rafiki yake Adola saivi nasearch for new members.

Akanambia hilo mbona nalijua toka muda sana, nikasema ndio uache kuniita shem tupishe maisha mengine yaendelee

Akanambia mimi nakuita shem sio kwa Adola ni kwa rafiki yako Josh. Kwani hakukwambia kuwa tumeanza kudate.

Weeeeeeeeeee, weeeee, weeeee.

Anyway kumuuliza Josh kuhusu ilo akawa anasema lemi teli you samusing (let me tell you something) kale kasauti mnakajua, kama hukajui nakaweka status WhatsApp na facebook ukimaliza kusoma nenda kakaone.

Basi bhana wiki ijayo ni harusi ya Josh na Purity.

Nitamuomba Dj niingie na wimbo wa sio mwana sio mwana huyo sinichi sio mwana,😭😭😭 sijasema nina wivu mimi ila Josh......

Kitu najaribu kukuelekeza hapa ni kwamba wife wako yupo sehemu yoyote huenda huyo shemeji yako ndio wife& husband wako we jaribu bahati yako kama Josh.

🥲🥲🥲 Naandika huku naugulia maumivu ukicheka block inakuhusu.
1736933997208.jpg

Pichani ni mimi baada ya kuambiwa Josh ndio sababu ya mimi kuitwa shem na sio Adola 😭😭😭

C&P Mtandaoni
 
Back
Top