Advertise here

Uzi Wa Kijobless Na Mbinu Za Kidgree: Kuna kipindi maisha yalinifanya niitwe King Sammy

Kasomi

JT Founder
UZI WA KIJOBLESS NA MBINU ZA KIDGREE

Kuna kipindi maisha yalinifanya niitwe King Sammy, ilhali sikuwa hata na kiti cha mstatili nyumbani. Nilikuwa mtaa flani Tabata.

Kipindi ambacho nilikuwa nikipata afu tano nahisi kama nimepokea sms ya

"umeshinda jackpot ya SportPesa"

Sasa mimi nilikuwa jobless halisi, ila nilikuwa na ndoto kubwa kuzidi hata chumba nilichopanga.

Naamini nilizaliwa kuoa mrembo mwenye kazi ya bank au NGO. Sio hawa warembo wa mtaani wenye maisha magumu kuliko hata mfupa.😂

Siku moja nikakutana na binti mrembo sana hapa hapa facebook.

tumuite Sandra (jina la kubahatisha tu). Huyu binti alikuwa na kila kitu, beauty, brains, na bio iliyoandikwa "Self-made boss babe, I don't chase, I attract".

Kwakweli sijawahi kumuona mrembo kama yule facebook nzima😁😁 au mnataka nimtag.

Nikaanza kum-inbox.

Mimi;Hi Sandra, una smile ya kutuliza shinikizo la damu.

Yeye:“Hahaa thanks, do I know you?”

Mimi:“Sidhani kama unamjua future husband wako, lakini ndio najitambulisha sasa.”

Ujasiri wangu haukuwa kutoka moyo, ulikuwa kwa sababu nilikuwa nimeshiba supu ya miguu ya mbuzi na vitunguu saumu.

Basi tukaanza kuchati, nikawa namsifia mpaka nikakaribia kumuomba apokee tu posa online.

Siku moja akasema anataka kuonana na mimi physically. Hapo ndipo nikajua hii ndo mitihani ya kidunia wanayokutana nayo watu wanaoenda kukutana na wadada wa facebook na hawakuambiaga.

Tatizo: sina nguo ya maana, sina hela ya saluni, na kiatu changu kimeachana na sole upande wa kushoto.

Nikasema akili kumkichwa, nikaenda kwa fundi viatu nikamwambia anishone haraka, akanipa bei nikamwambia

"nitalipa kwa exposure". Mifumo na ujanja ujanja tu😂

Nikavaa shati la mshikaji wangu Shadrack, suruali ya roommate wangu Mrote, na nikatembea kwa miguu kilomita mbili ili nijidai niko fit.

Hata angeniuliza ningemwambia me ntu ya mazoezi bhana.😎

Tukakutana Mlimani City.

Nilipofika nilimwona Sandra... JAMANI! Huyu binti ni kama alitengenezwa kwa specs za watu wa Qatar.

Nilikaribia kupoteza fahamu kwa urembo, ni kama ni malaika aliyesahaulika duniani.

Nyie Mungu anajua kuumba bhana🙌🏿🙌🏿

Tukaanza mazungumzo:

Sandra:“Sammy, you look... different.”

Huyu mrembo kwake kiingilishi sio tatizo si hata nyie mnaona😁

Mimi:“Unajua mimi kila siku ni new version ya mimi. Leo ni Sammy pro stable release.”

Sandra:“Unafanya kazi gani?”

Hapa nikawaza kazi ni kazi hata kuview status za watu WhatsApp ni kazi.

Mimi: “Nafanya kwenye digital sector... nina ushawishi mkubwa WhatsApp na Telegram. Niko kwenye peer-to-peer motivational business.”

Kiukweli hata mimi sijui ni kazi gani hio naonaga tu watu wa digito wanaisemaga.

Akanichekea tu.

Tukakaa, akaagiza smoothie ya 12,000, mimi nikaagiza maji ya 2000.

Alivyosema: “Tuletewe bill.” Nilijifanya nachukua simu, nikajifanya napokea call:

“Hallo? Daktari? Aisee shikamoo... nini?! Damu ya mguu imepanda juu?! Sasa damu ya miguuni inaenda kichwani kufanya nini, Sawa nakuja sasa hivi dakika mbili!”

Nikanyanyuka kwa haraka, nikamwambia Sandra:

“Nisamehe bill... usiwaze. Ila naitwa hospital haraka, kuna kesi ya ukoo.”

Nilitoka mbio kama naenda kufufua maiti. Toka siku hiyo Sandra alinitumia tu emoji ya moja tu tumbili anajifunika macho na hajanijibu tena hadi leo.
Hio emoj ndio ile ya kingedere kuficha sura🙈🙈🙈🐒

Nilijaribu kujielezea kwamba ilikuwa ni kesi ya ukoo, ningechelewa ningepata laana za ukoo lakini hakuwahi kunielewa akanipa na block juu 🥹🥹

Moral of the story:

Ukiona mrembo wa mtandaoni anakuita mlimani city, we chaguo sahihi zaidi ni kuto kwenda kama huna hela.

Na kama huna kazi, jifunze kuitwa "Digital Consultant" maana hata kuchat WhatsApp ni kazi ya kidigreee!
Ukisema ni kamba NAKUBLOCK kama Sandra alivyoniblock.🙈🙈

Pichani ni mimi baada ya kusikia swala la bill👇👇😂
1744542667457.jpg


Credit: Crarency Sanga
 
Back
Top