Advertise here
Nimeona post ina anuani, ''Maji Maji Rebellion.''
Sijakipenda kichwa hiki cha habari.

Hii mosi pili nimeona uandishi wa kejeli kwa mashujaa wa Vita Vya Maji Maji.

Kwa ajili hii naweka hapo chini makala niliyoandika kuhusu historia ya Tanganyika ambamo ndani yake naamimi yamo mambo muhumu ya kujifunza ambayo yatamsaidia msomaji kufuta kebehi na kejeli yoyote siku zijazo ambazo zitaelekezwa kwa wapiganaji wa Vita Vya Maji Maji:


Katika nchi za Afrika ya Mashariki ukabila kutoka wakati wa ukoloni ulikuwa ni tatizo Kenya na Uganda.

Kenya tatizo la ukabila liikuwa kati ya Wakikuyu na Wajaluo.
Tanganyika hapakuwa na tatizo la ukabila.

Hapakuwa na makabila ambayo walikuwa wanasigana.
Tatizo la Tanganyika toka ukoloni lilikuwa udini.

Kenya na Uganda hapakuwa na tatizo la udini kwa kuwa Ukristo ndiyo ulikuwa umetamalaki ka dini kuu.

Waislam walikuwa wachache Kenya na Uganda kiasi hawakuwa tishio.

Tanganyika ilikuwa na Waislam wengi wa kuonekana.
Natumia neno, ''tishio,'' kwa maana ya kuwa walikuwa na uwezo wa kuutikisa ukoloni.

Wajerumani walionja nguvu hii katika Vita Vya Maji Maji.
Waingereza waliishuhudia nguvu hii wakati wa siasa za utaifa baada ya Vita Vya Pili katika harakati za kupigania uhuru.

Ilikuwa tabu kuwatenganisha Waislam na joto lililokuwa linafukuta ndani ya TANU dhidi ya Waingereza.

Udini uliokuwapo Tanganyika wakati wa ukoloni ulikuwa kutoka kwa Waingereza na Wamishionari kutoka mataifa kadhaa ya Ulaya ambayo serikali iliwaachia kutawala elimu na wakaitoa elimu hii kwa kuwabagua Waislam.

Waingereza walipoja kuitawala Tanganyika baada ya kuondoka Wajerumani baada ya Vita Kuu Vya Kwanza, Wajeruamani walikuwa wameshafanya kazi ya kutosha ya kuiweka Tanganyika ndani ya mamlaka mbalimbali za Kikristo.

Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika mamlaka mbalimbali za Kikristo kutoka nchi tofauti za Ulaya. Kanisa Katoliki ambalo ndilo lenye nguvu zaidi, lilikuwa tayari limeshajikita Tanganyika.

White Fathers walikuwa wapo Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba; Holy Ghost Fathers walikuwa Morogoro na Kilimanjaro; Benedictine Fathers walikwepo Peramiho na Ndanda; Capuchin Fathers walikuwepo Dar es Salaam; Consolata Fathers walikuwepo Iringa na Meru; Passionist Fathers walikuwa Dodoma; Pallotine Fathers walikuwa Mbulu; Maryknoll Fathers walikuwapo Musoma; na Rosmillian Fathers walikuwa Iringa.

Hii ndiyo sababu harakati za kupambana zilipoanza Waislam walikuwa kitu kimoja jicho lao likimlenga adui ambae hawakuwa na shida kumtambua.

Waislam hawakupata hata siku moja kumwangalia Mwafrika Mkristo kama adui.

Hii ndiyo sababu Julius Nyerere aliweza kuchaguliwa kuongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na akawa kipenzi cha Waislam.

Sasa tuangalie nyuma tutazame mwanzo wa harakati za kupambana na ukoloni.

Ukienda Kilwa na Songea katika kumbukumbu za Vita Vya Maji Maji majina haya ndiyo utayokutananayo kuwa walinyongwa na Wajerumani kwa kunyanyua silaha dhidi yao:


1649736278522.png

1649736317751.png


Waingereza wao walipambana na hao unaowaona hapo chini:

1649736350944.png

Baraza la Wazee wa TANU 1957​
 
Last edited:
Back
Top