Advertise here

Trump aliagiza Jeshi lifanye Mashambulizi ya kuua kundi la Kigaidi Nigeria

Kasomi

JT Founder
donald-trump-5-gty-gmh-250821_1755813112349_hpMain.jpg

Rais wa Marekani Donald Trump amesema ameagiza Jeshi la nchi hiyo kufanya mashambulizi “makali na ya kuua” dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu (ISIS) Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria.

Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa Truth, Trump alilitaja kundi hilo la Kiislamu kama “takataka za kigaidi.”

Kwa mujibu wa Trump, sababu ya mashambulizi hayo ni hatua za kundi hilo kuwalenga “hasa Wakristo wasio na hatia,” ambazo alisema zimefikia viwango “ambavyo havijashuhudiwa kwa miaka mingi.”

“Chini ya uongozi wangu, nchi yetu haitaruhusu ugaidi wa Kiislamu wenye misimamo mikali kustawi,” alisema Trump.

Nigeria imekuwa ikikabiliana na uasi hatari wa makundi ya Kiislamu yenye itikadi kali katika maeneo yake ya Kaskazini-Magharibi kwa miaka kadhaa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Maitama Tuggar ameiambia BBC ni "operesheni ya pamoja" inayolenga "magaidi," na "haina uhusiano wowote na dini fulani."
 

Similar threads

Back
Top