Kasomi
JT Founder
Mwanaume anayefahamika kwa jina la Kelvin Mdolo (42) mkazi wa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, amekutwa kwenye nyumba ya kulala wageni (Guest) akiwa na kipande cha sehemu za siri ya mwanamke na alipohojiwa na Jeshi la Polisi amedai kuwa huwa anakitumia kiungo hicho katika shughuli zake za uganga wa Jadi mkoani humo.
Jeshi la polisi mkoa wa Kagera limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na limesema mbali na mtuhumiwa huyo kukutwa na kiungo hicho amekutwa na viungo vingine vya binadamu, ikiwemo mfupa mmoja wa taya, kipande cha moyo, kipande cha nyuma cha kondo la uzazi wa mwanamke.
"Kilichokamatwa ni nyama ya sehemu za siri za mwanamke ambayo imekaushwa, lakini pia hata hilo kondo la nyuma la kwenye mfuko wa uzazi na lenyewe limekaushwa...
...mwanaume huyo alipohojiwa zaidi kuwa kavitoa wapi [Viungo Hivyo] alieleza kuwa alipewa na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Randani Mlomo ambaye ni Muhudumu wa chumba cha kuifadhia maiti kuwa ndiye aliyempatia viungo hivyo huko Mbozi mkoani Songwe [alipokuwa anaishi] Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Blasius Chatanda akitoa taarifa hiyo kwa Umma Julai 02, 2025.