Kasomi
JT Founder
ChatGPT imeweka sehemu mpya ya ChatGPT Search ambayo itakuwa inafanana na Google kwa kusaidia kutafuta vitu mtandaoni lakini kwa kutumia akili bandia.
Mwanzo wa mwaka huu tuliwahi kutoa tetesi kuwa OpenAI na mpango wa kuweka mfumo ambao utashindana na Google. Mwezi Oktoba ikaanzisha rasmi mfumo wa ChatGPT Search ambayo unafanana na Google Search lakini ilianza kwa baadhi ya watumiaji kama sehemu ya majaribio.
Sasa watumiaji wote wanaweza kutumia ChatGPT Search katika app ya ChatGPT.
ChatGPT Search inasaidia kutafuta na kujibu maswali mbalimbali kwa kutumia database ya sasa (latest informations) zilizopo mtandaoni na kuonyesha links za vyanzo vya taarifa kwa kutumia akili bandia ambayo inaweza kutafuta vitu mtandaoni kwa umakini kuliko Google.
Google pia tayari imeanza kuweka mfumo wa akili bandia katika kusaidia kutafuta vitu mtandaoni ili kushindana na ChatGPT ambayo imekuja kwa speed sana kwa sababu ya matumizia ya akili bandia.