Nyongeza Katika Historia ya Ng'wanamalundi

Kasomi

JT Founder
NYONGEZA KATIKA HISTORIA YA NG'WANAMALUNDI KUTOKA KATIKA NILIYOSIMULIWA NA WAZEE WANAGU.
30

Anaandika Faida Potea,

Sijui tuseme ni asili au ndiyo mambo ya kizungu yametutawala, miaka ya nyuma hasa huku usukumani ilikuwa ni kawaida mkimaliza kula chakula cha usiku babu au baba ni lazima awasimulie mambo ya kale, yaweza kuwa ni ya watu maarufu au ukoo wenu ulikotoka.

Lakini leo hayo mambo yanaenda yanapotea, ndiyo maana watu wengi hawajui hata ukoo wake ulitoka wapi. Haya niliyoandikia ni kutoka katika simulizi nilizo simuliwa na Babu zangu mengine nimesimuliwa na wajukuu wa Ng'wanamalundi kabisa.

Ngw'anamalundi alikuwa ni mtu muugwana sana asiyependa mkuu, ila ukimkosea alikuwaga mkali sana. Alikuwa na watoto wawili, Sitta na mdogo wake aliitwa Ngasa. Hawa watoto wake walikuwa watundu sana kiasi kwamba kila siku ni mwendo wa kuletewa kesi.

Kutokana na Madawa aliyokuwa nayo alikuwa haruhusiwi kumpiga mtu yoyote au kumsonta, akwa akiletewa kesi anamwambia mke wake bhatulage abhana bhko, akimanisha wachape hao watoto wako.

Siku moja akaletewa kesi kwamba hao vijana wake wameenda kufyeka shamba la mtama la jilani yake, siku hiyo alichukia sana akawafoka sana, unaambiwa yale maneno tu aliyotamka waliugua nusu kufa.

Baada ya hapo akaamua kuwatenganisha, akamtoa Ngasa na kumpeleka kwa rafiki yake Mtemi Makwaya wa Utemi wa Bhusia huko Ukenyenge Wilaya ya Kishapu na akawapa onyo kwamba kuanzia leo hamtakiwi kuonana tena mapaka kufa kwenu.

Akabaki na Sitta hapo nyumbani ndipo vurugu zikaisha, waliishi na onyo hilo maisha yao yote na hata kwenye Mazishi alishiriki Sitta tu, Ngassa alikuja kuhani na hakumkuta kaka yake maana alimpisha ili wasionane.

Baada ya kifo chake Sitta ndiyo alikabidhiwa mikoba ya baba yake, hakukaa sana hapo kijijini kwao Seke Idadi. Akahamia kijini cha Ngw,alugulu wilaya ya kahama akaendelea kuwa mganga wa jadi japo hakuwa na uwezo kama baba yake.

Ngasa yeye alioa huko huko Ukenyenge na akaishi huko huko. Maisha yao yote kaka mtu akitaka kwenda kwa mdogo wake anatuma kwanza watu mwezi mmoja kabla wanapeleka taarifa kuwa mwezi ujao anakuja ili mdogo wake afanye maandalizi ya kumpisha. Na mdogo mtu naye hivyo hivyo akitaka kwenda kwa kaka yake.

Sitta akiwa ngw,alugulu mke wake akapata mimba, alipokaribia kujifungua mtoto aliongelea tumboni na kuwambia Nishoshagi gunzengo go gw,aguku nagabyalilwe kwene, nagujubhiza mfumu ntale. Akiwa na maana kwamba Niridisheni nikazaliwe kwenye makazi ya babu yangu, nitakuwa mganga mkubwa wa jadi.

Sitta na mke wakarudi Seke Ididi na haukuisha hata mwezi akazaliwa mtoto wa kiume akiwa ameshikilia vitu kama mizizi kwenye mkono wake wa kulia. Na wakampa jina la JISHOSHA.

Sitta na mke wake walikaa seke kwa miaka kadhaa baadae wakarudi Ngw'alugulu na kuendelea na maisha yao. Huyu mtoto Jishosha alipofikisha umri wa kwenda shule wakampeleka akaanza kusoma, lakini akawa ni mtundu Balaa.

Akienda kuchunga ng'ombe za baba yake anachungia kwenye mashamba ya watu, wanaleta mashitaka kwe baba yake. Wakienda kuangalia shamba lilivyoharibiwa wanalikuta lipo vizuri tu halina hata uharibifu hata kidogo, ila wakitoka tu akabaki mwenye shamba linaonekana limeharibiwa.

Ilifikia hatua baba yake akawa analipa tu faini ili kuepuka ungomvi na wananzengo, Baadae Jishosha akaamua kuwa mtu wa dini akabatizwa akaitwa Zakaria. Hapo nidpo miujiza yake ikakomaa na hakuweza kuwa mganga wa jadi tena. Aliishia kuwa askari polisi tu.

NAOMBA TUISHIE HAPO..! ASANTENI SANA.

Kusoma historia yake bonyeza hapa
 

Similar threads

Back
Top