Simulizi
Member
NALILIA WATOTO WANGU
Nimekuwa kwenye mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 8 bila kujua kuwa ana mke wake.
Mwanaume huyu tulikutana miaka 8 iliyopita alipokuja nchini kwa likizo akitokea Canada anapoishi na kufanya kazi.
Alinipenda mno na hakuwa mtu wa maneno mengi zaidi ya kuniambia mara kwa mara "nakupenda sana Melina wangu".
Katika mahusiano hayo nilipata ujauzito na nilipomwambia nilidhani angehamaki lakini alifurahi sana na kuzidisha upendo wake kwangu. Hatimaye likizo yake ndefu ilipoisha alirudi Canada huku akinitaka niwe mvumilivu kwani anaandaa mazingira ya kurudi nchini moja kwa moja ambapo tutaweza kufunga ndoa na kuishi pamoja na mtoto wetu.
Aliporudi Canada aliendelea kunitunza vizuri kwa kutuma pesa mara kwa mara hadi nilipojifungua mtoto wangu wa kwanza tuliyemuita Jian.
Baba Jian alikuwa na kawaida ya kuja nchini mara mbili kwa mwaka huku akinitumia pesa za matumizi yangu na mtoto ya kila mwezi. Niliendelea kukaa nyumbani kwetu kwa matarajio kwamba siku si nyingi atarudi tufunge ndoa na kuanza maisha yetu. Baadae Jian alipofikisha miaka miwili nikapata ujauzito mwingine. Nililea mimba bila shida hadi mtoto wa pili Julian alipozaliwa.
Siku moja Baba Jian aliniambia: "Melina wangu, nataka nijenge kabisa nyumba yetu hata kama ndogo, ili nikija tupate pa kuanzia tusikae wote kwa wazazi wako". Niliona ni wazo zuri na nikaona ni mwanaume anayejielewa. Alianza kutuma pesa za ujenzi na ndani ya miaka miwili nyumba ikawa imekamilika. Akanunua fenicha nzuri na vitu vyote vizuri tayari kuanza maisha pamoja.
Kuna siku Baba Jian akanipigia simu na kuniambia:
"Melina wangu, nimepandishwa cheo huku na mshahara wangu umekuwa mkubwa sana. Mimi nimeghairi kurudi huko kwa sasa nataka nije kuwachukua wewe na watoto mje tuendelee kuishi huku Canada"
Kwa kweli nilifurahi sana na hata wazazi wangu walifurahi mno.
Basi maandalizi ya safari yalianza na tukaanza kufuatilia passport. Tulipopata alikuja na kuanza kufuatilia mambo ya viza. Siku hiyo akasema anaenda kufuatilia viza zetu pia anawapeleka watoto kwanza peke yao ubalozini kwa ajili ya viza na kuwatambulisha na haina haja ya mimi kwenda. Basi akaenda nao na wakapata visa. Kisha akaniambia viza yangu mimi itatoka baada ya mwezi mmoja kwani tayari ameshanifanyia application. Kwa kuwa sikuwa najua lolote kuhusu utaratibu wa kuomba viza basi sikuwa na mashaka yoyote. "Melina wangu, Acha nitangulie na watoto kisha baada ya mwezi mmoja wewe utakuja peke yako kwani utashindwa kusafiri peke yako baby?"
"Hapana nitaweza kabisa"
Siku ya safari ilifika na mimi na wazazi tuliwasindikiza yeye na watoto Airport na kuagana kwa furaha nikijua baada ya mwezi mmoja nami viza yangu itatoka na nitaungana nao.
Walisafiri salama hadi Canada na kunijulisha kuwa wamefika salama na nikaongea na watoto kwa video call wakiwa na furaha sana na kunisimulia jinsi walivyopaa angani na mambo waliyoona njiani.
Baada ya kufika Canada baba Jian mawasiliano yalianza kupungua, nikipiga simu hapokei, akipokea ananijibu kwa mkato na kudai hana muda wa kuongea. Aliacha kutuma matumizi na alikuwa hataki niongee na watoto. Mambo haya yalitokea kwa ghafla sana na kuniumiza sana nikijiuliza nimekosea wapi mbona hatujawahi kugombana?
Siku moja Baba Jian akanipigia simu na huku akiongea kwa sauti kavu isiyo na hjsia zozote aliniambia:
"Melina, kuna jambo naomba tuongee ila naomba unisamehe sana. Naomba unisamehe kwa muda niliokupotezea ila leo naomba nikueleze ukweli kuwa mimi ni mume wa mtu. Nina mke wangu nampenda sana ila hatukubahatika kupata watoto na ndipo tukakubaliana kuwa nije kutafuta watoto huko mbali na yeye yupo tayari kuwalea. Siwezi kuendelea na mahusiano na wewe wala kufunga nawe ndoa tena kama nilivyokuahidi. Usiwe na mashaka hawa watoto wataishi vizuri, watasoma vizuri, watalelewa vizuri na wewe utabaki kuwa mama yao. Nisamehe sana Melina kwa hayo yote na tayari nimekutumia milioni 20 kama kifuta machozi. Lakini pia hiyo nyumba niliyojenga nimekuachia ni yako. Ila kuanzia leo naomba usinifatute kwa heri wala shari wewe endelea na maisha yako na watoto wakikuwa wakubwa watakutafuta tu".
Nimelia sana hadi nafikiria kujiua. Naomba ushauri,
NIFANYEJE?