john achila mukumwa
Member
Je watoto kupatilizwa kwa ajili ya dhambi za wazazi wao?
Kitabu cha Ezekieli 18:20 kinatuambia, "Roho atendaye dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua ouvu wa mwanawe".
Watoto hawaadhibiwi kwa ajili ya dhambi zilizotendwa na wazazi wao; wala wazazi kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi za watoto wao. Kila mmoja wetu anawajibika kwa ajili ya dhambi zake.
Aya ya Ezekieli 18:20 inaonyesha wazi kwamba adhabu ya dhambi ya mtu hubebwa na mtu huyo mwenyewe.
Hata hivyo, kuna aya ambayo imesababisha baadhi ya watu kuamini kuwa Biblia inafundisha adhabu kuhamishika kizazi hadi kizazi, kwa ajili ya dhambi. Tafsiri hii siyo sahihi.
Mstari katika suala hili ni kutokana na Kutoka 20:5, ambapo unasema kuhusu kumbukumbu ya sanamu: "Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mini, BWANA, Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizaki cha tatu na cha nne cha wanichukiao".
Mstari huu hauzungumzii hasa adhabu, bali matokeo. Unasema kwamba matokeo/effect ya dhambi za mwanadamu yanaweza kuhisika hata baadaye. Mungu alikuwa akiwaambia Israeli kuwa watoto wao watahisi athari za kizazi cha wazazi wao, kama matokeo ya asili ya uasi wao na chuki kwa Mungu. Kwa mfano, watoto ambao walilelewa katika mazingira ya kuabudu sanamu pia watafanya ibada ya sanamu, hivyo kuanguka katika mfano imara wa uasi.
Katika Biblia, neno kupatiliza halina maana ya kufuatilia, bali lina maana ya “kuadhibu”. Mfano, badala ya kusema “fulani, ameadhibiwa na Mungu, unaweza kusema fulani amepatilizwa na Mungu”.
Lakini, swali la kujiuliza ni je, Mungu huwa anaadhibu (anapatiliza) watu?
Jibu ni ndiyo. Huwa anatoa adhabu. Anawapatiliza waovu, vile vile na wema, endapo wakitoka nje ya mstari.
Lakini siku zote adhabu za Mungu lengo lake ni ili sisi tutubu na si kutukomoa au kutukomesha, kama sisi wanadamu tunavyokomeshana.
Kupatiliza hadi kizazi cha nne, maana yake ni kuwa Mungu anatoa adhabu hata kwa kitukuu au kilembwe, endapo wataendelea kutenda makosa ambayo mababu zao walikuwa wanatenda. Hiyo isichukukiwe kuwa ni kufuatilia ili kufanya kisasi, la hasha. Hiyo siyo maana yake. Bali ni adhabu zinazotolewa kawaida. Kama kizazi fulani hakikutenda kosa lo lote, Mungu hawezi kuadhibu kitukuu au kilembwe, eti tu kwa vile babu zake walitenda kosa fulani, hapana.
Matokeo/athari/effect za kizazi cha uasi ilikuwa tu kupanda uovu, kwa kiwano cha ndani kiasi kwamba ilichukua vizazi kadhaa baadaye kuuondoa. Ni kwa sababu kizazi kimoja hurithi kwa kuona na kutenda kosa lile lile kutoka kizazi kilichotangulia. Mungu hatufanyi kuwajibika kwa ajili ya dhambi za wazazi wetu, lakini sisi wakati mwingine huteseka kutokana na matokeo ya dhambi za wazazi wetu, kama Kutoka 20:5 inavyoeleza.
Ni sisi binadamu wenyewe ndio hung'ang'ania na kuendelea kuiga na kutenda matendo ya wazazi wetu, kupitia njia ya mila, utamaduni, au tabia. Na hii huendelea hadi hata kizazi cha nne, kabla ya kuondoka kabisa. Mfano wake ni kama vile leo, baadhi ya fasheni za kutenda mambo, hupotea baada ya kutendwa kwa muda mrefu na watoto na wajukuu.
Yaani, ukiabudu sanamu, kama babu yako au kama baba yako au bibi yako au mama yako, Bwana atakuadhibu wewe mzao wake kama na wewe utaendelea kuabudu sanamu kama babu zako. Lakini Mungu hawezi kuadhibu mjukuu wa babu aliyekuwa anaabudu sanamu, kama mjukuu huyo yeye hataabudu sanamu kama babu au bibi au mama yake alivyofanya. La hasha!
Kama mjukuu wa kizazi cha tatu au nne atafanya kosa ambalo babu yake alilitenda na kuadhibiwa, Mungu hawezi kuacha kumuadhibu mjukuu huyo au kitukuu hicho, eti kwa vile alikwishamuadhibu babu yake kwa kosa hilo hilo, la hasha. Atamuadhibu. Na siyo kwamba atamuadhibu kwa kosa la babu yake, hapana, ni kutokana na kosa lake mwenyewe alilotenda, hata kama ni kwa kurithi kosa aina ile ile kutoka kwa mababu/bibi/baba/mama zake.
Ni kwa mfumo au njia hiyo ndiyo Kutoka 20:5 inaongelea, lakini siyo vinginevyo. Siyo mpango wa Mungu kuadhibu kizazi/mtu eti kwa kosa la kizazi/mtu mwingine.
NI MUHIMU KUTOFAUTISHA HILO VIZURI ILI KUTOFANYA KOSA LA KUSIMSINGIZIA MUNGU.
Kama vile Ezekiel 18:20 anavyoonyesha, kila mmoja wetu anawajibika kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, na sisi lazima kubeba adhabu kwa ajili yetu wenyewe, wala si watoto wetu. Hatuwezi kushiriki hatia yetu na mwingine, wala mwingine kuwajibika kwa ajili yake.
Warumi 14:12 inasema: “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu”.
Hata hivyo, isipokuwa kuna sheria moja kuu kwa hili, na inatumika kwa watu wote. Mtu mmoja alichukua dhambi za watu wengine na kulipa adhabu kwa ajili yao, ili wenye dhambi waweze kuwa wenye haki kabisa na safi mbele ya Mungu.
Mtu huyu ni Yesu Kristo. Mungu alimtuma Yesu ulimwenguni ili kubadilishana ukamilifu wake kwa dhambi zetu.
"Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye" (2Wakorintho 5:21).
Yesu Kristo anachukua mbali adhabu ya dhambi kwa wale ambao huja kwake katika imani.
Hiyo basi, watoto hawawezi kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi za wazazi wao.
Ni kama asemavyo Ezekieli 18:20:
"Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake".