Advertise here

Fahamu Kitambulisho cha NIDA kilipo| Jinsi ya kuchukuliwa Kitambulisho cha NIDA (Kitambulisho cha Taifa)

Kasomi

JT Founder
Jinsi ya Kufahamu Kitambulisho chako kilipo au iwapo Kitambulisho chako cha Taifa Kimeshachapishwa

1)Tafadhali Piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja namba 0232210500 kuanzia saa 01:30 asubuhi hadi saa 09:30 jioni, kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kufahamishwa iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua au
2)Fika kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA wilayani.

Ukiarifiwa kuwa Kitambulisho chako Kimesha chapishwa, utasubiri kupokea SMS ndipo uende ofisini NIDA kuchukua kwani kwa sasa vitambulisho vyote vilivyokuwa vimepelekwa kwenye Kata/Serikaliza Mitaa na wananchi husika hawakujitokeza kuvichukua ndani ya muda uliokuwa umetengwa na kuongezwa, vyote vimerudishwa ofisini. Tangu Januari 2025, Wananchi wanaendelea kugaiwa kwa kutumiwa SMS kwanza.

NIDA kwa kushirikiana na TCRA, itaweza kuwafikia waombaji wote wa Utambulisho wa Taifa hata wanaojisajili kwa sasa ama wanaohuisha vitambulisho vyao hata kwa wale walio badili Namba za Simu, NIDA itaweza kuwatumia SMS kupitia Namba zao zote za simu wanazo zitumia sasa. Iwapo bado kufikiwa, utafikiwa hivi punde.

SMS zinafungwa pindi siku 30 zikipita baada ya mteja kupokea SMS kutoka NIDA, ikimtaka kufika kwenye ofisi ya Usajili katika wilaya alikosajiliwa, kuchukua Kitambulisho chake.
Utumaji SMS unahusisha pia kundi la ambao wamesajiliwa hivi karibuni na wanaoendelea kujisajili, waliohuisha taarifa (marekebisho ya taarifa) ama kitambulisho (kilichopotea) na ambao wamerejesha vitambulisho vilivyofutika ili wachapishiwe vingine.
Shukrani.

Jinsi ya kuchukuliwa Kitambulisho cha Taifa (NIDA ID)
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imerahisisha suala la kuchukuliana Kitambulisho cha Taifa (NID) ambapo mtu, anayehitaji kuchukuliwa Kitambulisho cha Taifa, atapaswa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), aliyotumiwa na NIDA kwa mtu anayemtuma kumchukulia Kitambulisho.

Aliyetumwa kumchukulia mtu mwingine Kitambulisho, anapaswa kuonesha SMS, aliyotumiwa na mmiliki(mwombaji) wa Kitambulisho, afikapo kwenye ofisi ya ya NIDA, katika wilaya alikosajiliwa mwombaji, kwa ajili ya uthibitisho kabla ya kupatiwa Kitambulisho hicho.
Mtumishi anayehusika na Kugawa Vitambulisho, akithibitisha na kujiridhisha kuhusu uhalali wa SMS hiyo, ataendelea na hatua ya kutoa Kitambulisho kwa mhusika aliyetumwa.

Mfumo huu umelenga kuondoa urasimu katika kuchukuliana Vitambulisho ili kurahisisha Utoaji wa Vitambulisho hivyo hasa kwa wananchi waliohama makazi, walio nje ya nchi, wagonjwa, wazee na wanaoshindwa kufika kwenye wilaya husika kwa sababu nyinginezo.
Upatapo Ujumbe Huu Tafadhali Mwarifu na Mwingine!
Kitambulisho cha Taifa kwa Maendeleo Yako Mwananchi na Taifa kwa Ujumla!

Nahitaj kujua kitambulisho changu kilipo
 
Back
Top