Kasomi
JT Founder
Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro amekamatwa alfajiri ya leo Jumamosi na wanajeshi wa Delta Force, kikosi cha operesheni maalum cha Jeshi la Marekani. Tukio hili limetokea katika muktadha wa operesheni kubwa inayohusisha vikosi vya Marekani, ambavyo vimejizatiti katika kushughulikia mishemishe ya kiusalama za kiwango cha juu.
Delta Force ni kikosi cha usalama cha Jeshi la Marekani, kinachotumika kutekeleza misheni hatarishi, ikiwa ni pamoja na kupambana na ugaidi, kuokoa mateka, kufanya mashambulizi ya moja kwa moja, na shughuli za ujasusi wa kijeshi. Kikosi hiki mara nyingi kinahusika na malengo ya kipekee na yenye umuhimu mkubwa kimataifa.
Umaarufu wa Delta Force uliongezeka mwaka 2019 wakati kikosi hicho kiliongoza operesheni iliyomuua kiongozi wa zamani wa Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi, hatua ambayo ilithibitisha uwezo wa kikosi hicho katika kushughulikia operesheni ngumu na za kimataifa.
Operesheni ya kukamatwa kwa Rais Maduro inatajwa kuwa ni sehemu ya juhudi za Marekani kuendeleza kampeni yake dhidi ya serikali ya Venezuela, ambayo imekuwa ikikosoa hatua za Marekani kwa muda mrefu.
Hamound Marcel ambaye ni Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na diplomasia anafafanua Zaidi.
Tazama video hapa