Advertise here

Kasomi

JT Founder
HISTORIA YA DR. JOHN THOBURN WILLIAMSON

Sehemu ya 1

1768161737526.jpg

John Thoburn Williamson alizaliwa huko Montfort, Quebec mnamo tarehe 10 Februari 1907, ni wapili kuzaliwa kati ya watoto wanne kwenye familia yao. Baba yake, Bertie J Williamson,alikuwa ni Mscotland ambaye alikuwa amehamia Canada kutokae Ireland. Mama yake, Rose C Boyd alikuwa Mfaransa.

Mnamo mwaka 1919 Familia hiyo ilihama kutoka Montfort na kuhamia Montreal ambapo John alienda shule ya upili ya Macdonald huko Ste Annede Bellevue. Kutoka hapo aliingia Chuo Kikuu cha Mc Gill mnamo 1925 ambapo alisoma sheria. lakini baadae
aliamua kubadili masomo na kusoma jiografia.

Alipata shahada ya BA mnamo 1928, Shahada ya Uzamili ya Sayansi mnamo 1930 na Shahada ya Uzamivu mnamo 1933. Profesa wake wa zamani wa Jiolojia, Dk Richard Graham, alialikwa Johannesburg kukagua ardhi ambayo kampuni ya De Beers walita kakufanya uchunguzi. Williamson aliongozana na Dk Graham na kutoa hotuba fupi katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand.

Baada ya hapo John T. Williamson alialikwa kujiunga na kampuni ndogo ya De Beers Consolidines Mines, kama mtaalam wa jiolojia ambapo alikubali.
Kampuni hiyo ilikuwa ikifanya utafiti wa shaba katika nchi ya Rhodesia ya kaskazini mashariki, (Zimbabwe)
Dr Williamson aliwafuata wakurungezi wa De Beers na kuwaomba wamdhamini akafanye utafiti wa madini ya almasi katika nchi ya Tanganyika lakini walimkatalia na akaamua kujiuzulu kufanya kazi katika kampuni hiyo.

Dr Williamson aliamua kujiunga na Kampuniya Tanganyika Gold and Diamond Development
mnamo1935, akifanyakazi chini ya mtaalam wao mkuu wa jiolojia, Hank Le Tendresse, Mmarekani ambaye alimkubali Sana John Thoburn Williamson, Hata hivyo hakulidhika kufanyakazi Na kampuni hiyo. Mnamo Mei 1936 Dr Williamson alisafiri kwenda Mwanza kumtafuta Wakili mwenye asili ya Asia aliyekuwa anasheshimika sana, Bw Iqbal Chand Chopra KC. Walikutana tarehe 16 Mei1936.

Bwana Iqbal anasem,"Dr John Thoburn Williamson, aliletewa ndani ya chumba cha ofisi yangu akiwa na shati nyeupe na suruali ya khaki alitaka nimsaidie mambo ya kisheria ili aweze kufanya kazi yake ya utafiti wamadini ya almasi, na alihitaji kufadhiliwa pia."

Mnamo mwaka 1937 Kampuni ya Tanganyika Goldand Diamond Development ilisitisha shughuli za utafiti na kuanzia hapo Dr Williamson akawa huru kufanya kazi peke yake. Bwana Chopra aliungana na Dr Williamson na wakaanza kazi ya utafiti wa almasi. Waliaza utafiti pembezoni mwa Ziwa Victoria na Mikoa ya Magharibi bila mafanikio yoyote.

Alivumilia huko msituni na wavulana wawili wa aminifu wa Kiafrika, Bundala na James. Dr Williamson alikuwa ameweka kambi katika kijiji cha Kizumbi (mkoa wa shinyanga) na alikuwa anazunguka huku na huko akifanya utafiti wake na kisha kurudi kambini kwake. Na hakuwa na mtaji wa kutosha ilifikia hatua akabakiwa na dolla100 tu.

Hali hiyo ilimuweka njia panda kwani vifaa vyake vilikuwa vinahitaji matengenezo na wafanyakazi wake walikiwa wanamdai mshahara. Aliamua kupunguza wafanyakazi na kuamua kumalizia mchanga wake ili afungashe vilago aondoke zake. Wakati wanamalizia kuuosha mchanga huo alipata vipande viwili vya almasi vichafu kimoja kikiwa na uzito wa kareti 30, almasi hiyo ilimpa nguvu ya kuendelea na kazi.

ITAENDELEA
 
HISTORIA YA DR. JOHN THORBURN WILLIAMSON NA MGODI WAKE WA ALMASI MWADUI

Sehemu ya 2

Hali hiyo ilimuweka njia panda kwani vifaa vyake vilikuwa vinahitaji matengenezo nawafanyakazi wake walikiwa wakimdai mshahara. Aliamua kupunguza wafanyakazi na kuamua kumalizia mchanga wake ili afungashe vilago aondokezake.

Wakati wanamalizia kuuosha mchanga huo alipata vipande viwili vya almasi vichafu kimoja kikiwana uzito wa kareti 30, almasi hiyo ilimpanguvu ya kuendelea na kazi.

Mnamo mwezi wa February 1938 alisafiri mpaka mwabuki wilaya ya misungwi na alikaa huko kwa miezi kazaaakitafuta almasi, alipata lakini hazikuwa nyingi. Aliamua kurudi kizumbi kwenye mgodi wake na kuendelea na kazi, alifanya kazi bila kupata chochote kwa muda wa mwaka mmoja.

Mwaka 1939 mwezi wa 10 akiwa amekata tamaa ya kupata almasi, kijana wake Bundala yeye alikuwa anaendelea kuwasimamia wafanyakazi waliokuwa wakiosha mchanga. Williamson akiwa amelala
kwenye hema lake aliletewa na Bundala kipande cha Almasi kizuri sana chenye uzito wa kareti mbili.
Dr Williamson alifurahi sana na kumpa Bundala zawadi ya pesa.

Bundala alimuomba Williamson ruhusa azipeleke pesa zake nyumbani kwao katika kijiji cha Luhumbo (kwa sasa Mwadui ), Williamson alimkubalia kijana wake. Williamson alipatamatumaini tena ya kupata mkanda wa almasi maana aliamini kuwa lazima kuna sehemu karibuambayo mlipuko wa volcano ulipolipuka na kuzitoa hizo almasi.

Tarehe 6 mwezi wa 3 mwaka 1940 Bundala akiwa anatoka kijijini kwao kurudi kizumbi aliona vipande vinne vya almasi, ikiwemo ya rangi nyeusi pembezoni mwa mto akavichukua na kumpelekea boss wake Dr. Williamson. Dr Williamson alipoziona alichaganyiwa kwa furaha na maana alimasi hizo zilikuwa nzuri sana moja ikiwa na uzito wa carat 38. Akamwambia
Bundala ampeleke alipozichukilia, Bundala akiwa ameongozana na James na Dr. Williamson walifika sehemu ile na kuchimba kashimo kadogo wakatoa mchanga walipoosha walipata almasi nyingi sana.

Williamson alifurahi Sana na ndipo ndoto yake ya kuupata mlipuko wa volcano ikatimia. Alihamisha kambi yake kutoka kizumbi na kuileta Luhumbo na aliweka kambi chini ya Mbuyu, ( Mpaka leo Nembo Ya Mgodi Ni Mbuyu) kipindi hicho mtemi aliyekuwa anatawala hilo eneo alikuwa anaitwa NG'WADUBHI na eneo lake lilikuwa linajulikana kuwa BHUTEMI BHONG'WADUBHI. Dr. Williamson aliongea na mtemi akamruhusu kuanza kazi ya kuchimba almasi na alimuomba mtemi awahamishe wanakijiji waliokuwa wanakaa eneo hilo.
Eneo ulipo mgodi wa mwadui kilikuwa na vijiji vinane ambavyo ni ITUGUTU, NGW'ABHUKANGW'A, NGW'AGAGALA, ISHIDA, IBHELAMBASA, JINAMELI, LUHUMBO na GABHONDO. Mtemi pamoja na wananchi wake wakahama na kumwachia hilo eneo.

Mtemi akajengewa makazi mapya kijiji cha Utemini japo kipindi wanahamia walihama na jina lao la Luhumbo, baadae likapotea ikawa utemini wakimanisha kwa mtemi.

Dr. Williamson alifanya kazi kwa miaka kazaa wakiwa wanachimba watu na kusomba mchanga kupeleka
kwenye kamashine kadogo alikokuwa nako. Mwaka 1942 alienda Dar Es Salaam kusajili kampuni yake na aliisajili kwa jina la Williamson Diamond Ltd. Ikiwa na mtaji wa €20,000 na ikiwa na hisa 400 yeye akamiliki hisa 299 na akampa kaka yake anayejulikana kwa jina la Percy hisa 100 na rafiki yake Bwana Iqbal Chand Chopra akampa hisa 1. Huyu Mr Chopra ndiyo aliyemsaidi mambo ya kisheria kipindi anaenda kusajili kampuni yake.

Aliamua kuuita mgodi wake jina la Mwadui jina la mtemi aliye mkaribisha, kwa kisukuma alikuwa
anaitwa Ng'wadubhi. Jina la Ng'wadubhi lilimshinda kulitamka ndipo akaita Mwadui.

Notes:
Mpaka hapo tumeona mvumbuzi wa mgodi ni kijana wa Kisukuma Bundala lakini kwenye mgawanyo wa hisa hakupewa hata nusu hisa, na habari yake inaishia hapo hakuandikwa tena kwenye hii stori.

Wazee wetu huwa wanatusimulia alipewa ajira ya kudumu mgodini hapo na kujengewa nyumba na kununuliwa Ng'ombe wengi sana.

ITAENDELEA

Credit: Njile Nkuba Sitta
 
HISTORIA YA DR JOHN THORBURN WILLIAMSON NA MGODI WAKE WA ALMASI MWADUI

Sehemu ya 3

Aliamua kuuita mgodi wake jina la Mwadui jina la mtemi aliyemkaribisha, alikuwa anaitwa Ng'wadubhi. Jina la Ng'wadubhi lilimshinda kulitamka ndipo akaita
Mwadui.

Alipoona amekusanya almasi za kutosha ndipo. alipoenda kuuza kwenye soko la dunia na kuja
na mitambo ya kisasa. Alifanya utafiti na kugundua kuwa Mwadui ilikuwa na mkandawa "kimberlite "wenye hifadhi nyingi ya almasi. Ikiwa na ukubwa wa hakari 146, mkanda huu ni wa pili kwa ukubwa Duniani baada ya ule wa Mgodi wa Camafuca uliopo Angola.

Dr. Williamson mwaka 1946 alie kuchumbia katika familia ya kifalme huko Wingereza akitaka kumuoa Princess Margaret, akaambiwa huwezi kuoa kwenye familia yetu wewe ni masikini. Akajaribu kuwashawishi kuwa yeye ni tajiri anamilili mgodi wa almasi huko Tanganyika lakini akatoswa.

Alitoa zawadi ya Almasi yenye rangi ya PINK yenye uzito wa kareti 54.5 kwenye harusi ya Princess Elizabeth na Prince Philip mwaka 1947. Unaambiwa almasi hiyo ipo mpaka leo kwenye jumba la kifalme la Uingereza imewekwa pambo kwenye kofia ya Malkia, ilishachongwa ikabaki kareti 23.6. Mwaka1948 akafunga mkataba na serikali ya kikoloni ya Waingereza wa miaka 100 ( yaani 1948-2048. )

MAISHA NDANI YA MJI WA MWADUI.

Dr. Williamson akautengeneza mji mdogo wa Mwadui na kuwa moja kati ya miji bora sana kusini mwa jangwa la Sahara (MwaduiTownship). Kufikia mwaka 1947, Dr Williamson alikuwa amejenga nyumba bora za wafanyakazi, hospital ya kisasa, shule za msingi tatu, mbili za wafanyakazi wa kiafrika na moja ya wafanyakazi wa kizungu ambayo ndio ilikuwa moja ya "English Medium School" ya kwanza Tanganyika. Akajenga chuo cha Ufundi wa aina zote ndani ya mgodi kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi, chuo cha
kilimo na shule ya upili.

Huko kwao waliita "School Near The Equator". Ilikuwa shule bora na ya kisasa. Dr Williamson akajenga uwanja wa ndege wa kisasa ndani ya mgodi mwaka 1948 akanunua ndege mbili za mwanzo aina ya Dakota DC3 na Cessna 180 wakati huo hata serikali ya Kikoloni ya Muingereza ikiwa haina wazo la ndege, wakati serikali ya Tanganyika ikiwa haina uhakika wa
uwanja wandege kupokea ndege kubwa aina ya Dakota DC4.

Dr Williamson alikuwa tayari na uwanja huo, ambapo wageni toka London Uingereza, ndege zilitua Malta, Khartoum-Sudani na baadae Nairobi (Wakati huo ukiitwa Embakasi Airport) na baadae kuchukuliwa na ndege moja kwa. moja mpaka Mwadui Shinyanga, ambapo Serikali ya Kikolonii likuwa na afisa mmoja wa uhamiaji. Dr Williamson alijenga kanisa na msikiti bora na wakisasa kwa ajili ya wafanyakazi
wake.

Wakatihuo, usafiri pekee wa watumishi wa serikali ya Kikoloni ilikuwa ni meli maarufu ya"The Braimer Castro" iliyokuwa inatoka Ulaya mpaka Mombasa. Yeye Dr Williamson na wafanyakazialioajili walikuwa wanapanda ndege kupitia Embakasi na baadae Mwadui. Williamson akajenga "Power House" yenye uwezo wa kuzalisha 900kw kwa mitambo ya diesel
na 750kw kwa Gas Turbine na hivyo kuwa na umeme wa uhakika kuliko hata mji wa Dar Es Salaam.

Dr Williamson alijenga "SailingClub", yaani Club inayoning'inia katika bwawa alilichimba eneo la Songwa. Hii ndio ilikuwa Club pekee inayoning'inia Kusini mwa Jangwa la Sahara. May 2 mwaka 1955, Gazeti Kongwela "The Cairns Post" (Est.1882) liliandika juu ya uwepo wa bwawa la Songwa, Mwadui-Shinyanga, Tanganyika. Gazeti hilo la Australia lilielezea bwawa la Songwa kama moja kati ya "Artificial dam" kubwa zaidi duniani, lenye uwezo wa kuchukua "two thousands million gallons of water". Mradi ambao hata serikali ya mkoloni iliushangaa.

Notes;
Hiyo picha ni Dr. Williamson akiwa na Kijana Bundala wakiwa katika harakati za kuitafuta almasi.

ITAENDELEA

Credit: Njile Nkuba Sitta
 
HISTORIA YA DR JOHN THORBURN WILLIAMSON NA MGODI WAKE WA ALMASI MWADUI

Sehemu ya 4

1768162788587.jpg
Mwadui kulikuwa na mfumo wa maji safi na maji taka yaliyotibiwa na wataalamu waliosomeshwa na mgodi. Huduma ya elimu ya watu wazima na elimu ya uchumi wa nyumbani "home economics" kwa wamama waliokuwa nyumbani. Kufikia mwaka 1970, karibu 97% ya wakazi wa mgodi huo ambao walifikia 16000 walikuwa wanajua kusoma na kuandika, na wamama wakiwa na ujuzi wa ushonaji, upishi nk.

Dr Williamson aliajiri mpishi maarufu toka Ufaransa, ambaye alikuwa akipika na kuandaa chakula katika "mesi" kubwa ndani ya mgodi wa Mwadui. Mfaransa huyo alifundisha wapishi wengi wa Kiafrika na alikuwa kama "chuo" cha wapishi wengi wa maafisa wa serikali ya kikoloni, na hata wapishi wa mwanzo wa Ikulu ya Dar es Salaam baada ya Uhuru, walipita katika mafunzo ya "mesi" ya Mwadui.

Kufikia mwaka 1950, Tanganyika ilikuwa na vyumba viwili tu vyenye hadhi ya kulala familia ya kifalme ya Uingereza, chumba kimoja katika Ikulu ya sasa ya Dar es Salaam na kingine kwenye "rest house" ndani ya mgodi wa Mwadui.
Mpaka kufikia mwaka1952 mgodi wa Mwadui chini ya Dr. Williamson ulikuwa umeajiri wafanyakazi 2770. Waafrika walikuwa 2600, Wazungu 110 na Wahindi 60.

Mgodi wa Mwadui chini ya Dr Williamson, uliweza kujenga kiwanja cha golf chenye mashimo tisa, ambacho kilikuwa ni moja ya viwanja vikubwa na vya kisasa Afrika nzima. Mwaka 1952, Dr Williamson alishawishi mpaka mashindano makubwa ya kombe la Malikia la Golf nchini Canada yafanyike Mwadui, kila kitu kilikubalika isipokuwa hali ya uwanja wa ndege wa Embakasi Kenya haukuwa sawa sababu ya vuguvugu la vita vya Mau mau lililotishia usalama wa kiwanja.

Swimming Pool za viwango vya Olympic tatu ndani ya mgodi Viwanja vya tennis, pamoja na viwanja vitatu bora vya mpira wa miguu vilivyokuwa na viwango
vya kimataifa vilijengwa ndani ya mgodi wa Williamson. Timu ya mpira wa miguu ya Mwadui Mining ilishiriki mashindano ya kitaifa kwa ubora mkubwa. Waamuzi wakongwe waviwango vya kimataifa kama Mshangama na Mashishanga (RC wa zamani ) ni matunda ya Dr Williamson.

Ustawi wa maisha ya mgodi na kushamiri kwa faida ya Dr Williamson kuliwauzi "wamiliki" wakubwa wa biashara ya madini ya almasi ambao ni De Beers Group of Co. Almasi ya Mwadui iliingia kwa kasi sana katika soko la dunia jijini London. De Beers wakashindwa kumdhibiti Dr Williamson na almasi yake, akafanya almasi ya Afrika Kusini kushuka thamani katika soko la dunia, njia pekee iliyobaki kwa DeBeers ilikuwa kumtaka Dr Williamson aungane nao katika
biashara.

Dr Williamson alikataa, akataka kuuendesha mgodi kwa namna yake, hakutaka kuwanyonya wafanyakazi wake, ndoto zake ilikuwa ni kuijenga "Quebec ndogo ndani yaTanganyika", alitaka kuonyesha thamani ya madini na maisha ya wafanyakazi kwa kuutumia mgodi wa Mwadui. Aliiishi Afrika Kusini na kuona jinsi wazawa wa kando ya migodi na wafanyakazi wasivyofaidika na madini katika ardhi yao.

Dr Williamson hakutaka hali hiyo itokee. Mkoloni na De Beers walichukia uamuzi wa Dr Williamson kuufanya mgodi wa Mwadui kama "Ulaya ya Afrika". Walim-fustrate kwa kukataa kuipokea almasi yake katika viwanda vya kuchonga almasi kule London (diamond Cutting).

Mwaka 1950, Serikali ya kikoloni kwa Shinikizo la familia ya Oppenheimer wakataka kuutaifisha
mgodiwa Mwadui iliuwe mali ya serikali ya mkoloni na si mtu binafsi. Hali hii ilimchanganya sana Dr Williamson, akawa mlevi wa kupindukia wa whisky ya Scotland, akawa "chain Smoker" na kwasababu alikuwa "bachelor" hakuwa na mtu wa kumtuliza mawazo.

Notes;
Baada ya kukataliwa kumuoa Princess Margaret Dr Williamson hakutaka kuoa tena na alichukizwa na kauli ya kuambiwa yeye ni masikini, akaamua kuwaonyesha kuwa yeye siyo masikini kwa kuijenga mwadui iwe kama ulaya. Na alihamishia makazi yake mwadui yaani mwadui ndiyo ikawa nyumbani kwake, ndiyo maana mwadui ilijengeka.

ITAENDELEA

Credit: Njile Nkuba Sitta
 
Back
Top