Kasomi
JT Founder
HABARI Baada ya kufanya operesheni, doria na misako katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kubaini, kuzuia na kutokomeza uhalifu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limefanikiwa kuwakamata wahalifu wanaotuhumiwa kwa tuhuma za wizi wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) la Hospitali ya Manispaa ya Musoma.
Taarifa ya tukio hilo ilitolewa na uongozi wa Hospitali ya Manispaa ya Musoma tarehe 25 Oktoba, 2025 majira ya saa 02:00 usiku katika Kituo cha Polisi Musoma mjini Mara. Taarifa hiyo ilieleza kuwa kwa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili STM 7830, ambalo lilibiwa katika eneo la maegesho ya Hospitali ya Manispaa ya Musoma.
Kupitia upelelezi wa taarifa hizo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara lilifanikiwa mara moja kuchunguza na kufuatilia kwa kina, hatimaye liwakamata kubaini namna gari hilo lilivyotolewa pamoja na eneo lilipokuwa limefichwa.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limefanikiwa kukamata gari hilo likiwa katika hatua za mwisho za kubadilishwa muonekano, kutoka gari la kubeba wagonjwa (ambulance) na kuwa gari la kibiashara la kubeba watalii ambapo taratibu za kisheria za kuwasilisha watuhumiwa hao mahakamani zinaendelea kukamilishwa.
Watuhumiwa waliokamatwa kuhusika na wizi huo ni:
Goodluck Steven Chacha mwenye umri wa miaka 26 na mkazi wa Tarime mjini
Karume Kimwel mwenye umri wa miaka 26 na mkazi wa Mkoa Arusha
Saidi Hussein Ramadhani mwenye umri wa miaka 39 na mkazi wa Engosengiu Arusha
Elias Joachim Lyimo mwenye umri wa miaka 53 na mkazi wa Arusha