JIFUNZE LUGHA YA KINGEREZA KWA AJILI YAKO AU MWANAO UKIWA NYUMBANI KWAKO

Emmanuel

New member
*JIFUNZE LUGHA YA KINGEREZA KWA AJILI YAKO AU MWANAO UKIWA NYUMBANI KWAKO*

Si kila mtoto anaweza kuelewa somo kwenye kundi la wanafunzi wenzake kama darasani. Wakati mwengine mtoto huyu anahitaji kufundishwa katika namna ambayo ni mahususi na kuendana nae, mbinu ambayo ni ngumu mwalimu kuitumia kwenye kundi la wanafunzi wengi.

Pia, umri na majukumu kuongezeka inakuwa vigumu wakati mwengine kuhudhuria darasani kusoma.

Kwa sababu hizi, ndio linapokuja suluhisho la kupata msaada wa mwalimu binafsi.

1. Je wewe unakabiliwa na changamoto ya lugha ya kiingereza na ungependa kuijua ili kukuwezesha kimawasiliano ya kibiashara na matumizi ya kawaida?

2. Au ni mwanao ambaye kufeli kwake si kwa kuwa hana uwezo darasani bali ni kuwa hana msingi mzuri wa lugha hiyo ambayo ndiyo ya kufundishia?

Ikiwa jibu ni ndiyo, Mwalimu binafsi ambaye atakayeweza kukusaidia kwa hilo amepatikana. Mwalimu ambaye;

1. Atakuja nyumbani kwako kukufundisha wewe au mwanao,

2. Ataandaa somo na mazoezi mahususi kwa ajili yako au mwanao kutatua changamoto inayokusumbua/inayomsumbua.

*FAIDA 4 KUKIJUA KIINGEREZA*

*1. Fursa:* Wapo watu wanaodai hakuna haja ya kujifunza lugha yoyote zaidi ya kila mtu au nchi ibakie na lugha yake. Huu ni ufinyu wa fikra kwa sababu kuu moja; lugha zinatofautiana ukubwa wa matumizi yake. Mfano lugha ya kiswahili kinatumika Tanzania na baadhi ya nchi Afrika lakini si dunia nzima. Hivyo ikiwa una malengo ya kutanua wigo wako wa kuwasiliana na watu wengine duniani huna budi kujua lugha itakayowaunganisha wote. Kiingereza ni miongoni mwa lugha 5 kubwa duniani na kutokuijua si tu unajinyima uwanda mpana wa kimawasiliano lakini pia unapitwa na fursa nyingi ambazo ungeweza kuzipata.

*2. Okoa fedha za kumwajiri mkalimani:* Kingereza ndiyo inayotawala dunia kwa sasa kibiashara (mikataba, lugha inayotumika kwenye bidhaa nyingi, n.k) na kimatumizi ya kawaida (simu yako unayotumia, michezo, filamu n.k). Kuna njia mbili ya kuweza kujua maana ya kile kinachoendelea katika hayo;

A. kujifunza lugha hiyo wewe mwenyewe (gharama pekee ni kutenga muda na pesa kidogo) au

B. kumuajiri mkalimani (itakugharimu pesa nyingi kulinganisha na njia ya kwanza).

*3. Uhuru na Kujiamini:* Ni mara ngapi umekuwa ukiona mzungu tu au mtu akikuongelesha kiingereza fyuzi zote kichwani zinakatika na kuangalia huku na kule kutaka msaada kwa mtu au ikiwezekana kuondoka kabisa mahali hapo? Au ni mara ngapi mwanao anatetemeka na kuogopa kushindwa kujibu maswali darasani kwa sababu hajui lugha hii?

Yote haya yanaweza kuepukika kwa kuijua lugha husika. Kujua kitu kunaongeza kujiamini na uhuru wa kufanya kitu.

*4. Usiri:* Umeshawahi kuweka siri yako wazi kwa mtu kisa tu ulimuomba akutafsirie ujumbe uliotumiwa kwa lugha tofauti? Sasa hebu fikiria kwenye suala la kuingia mkataba mkubwa kwa lugha ya kiingereza na wewe hujui kilichoandikwa kisha ukauweka wazi kwa mtu ambaye si sahihi.

*UAMUZI NI WAKO*
Unajua changamoto unazopitia au mwanao anazopitia kwa kutokujua lugha hii na umeshajua baadhi ya faida utazopata au mwanao atakazopata kwa kujua lugha hii. Maamuzi ni yako sasa ya kufanya uwekezaji.

Gharama za mwalimu kufundisha ni;
1. Tshs 40,000 kwa dakika 60 kwa siku

2. Tshs 114,000 kwa dakika 180 (siku 3 katika wiki)

3. Tshs 360,000 kwa dakika 720 (siku 12 katika mwezi)

*NB: Gharama zimezingatia ujuzi wa mwalimu, kiwango chake cha elimu, muda wa uandaaji wa somo na gharama za usafiri.*

Kwa Mawasiliano Zaidi
+255738-656333 (Piga Simu)
 
Back
Top