john achila mukumwa
Member
Lugha iliyotumika kati ya Adamu na Mungu kwenye bustani ya Edeni
Biblia haijataja lugha gani ilikuwa inatumika pale bustani ya Edeni.
Ingawa Mungu ana uwezo wa kuzungumza na sisi pasipo lugha na tukamwelewa, lakini ni wazi kuwa kulikuwa na lugha fulani iliyotumika, kwa sababu Mungu ametuumba sisi wanadamu tuwe tunawasiliana kwa njia ya kuzungumza, na hatuwezi kuzungumza bila lugha.
Adamu mwanadamu wa kwanza alivyoumbwa, ni tofauti na wengine tuliofuata. Sisi wengine safari yetu ilianzia katika matumbo ya mama zetu, lakini siyo Adamu. Adamu Mungu alimwumba mkamilifu, kwa maana kwamba hakuzaliwa wala hakurithi. Wala hakufundishwa. Yaani aliumbwa tayari ana maarifa kichwani mwake (Mwanzo 2:7).
Tofauti na sisi. Tunapozaliwa inatuchukua muda mrefu sana maarifa yaingie kichwani mwetu. Hadi tuweze kuelewa hiki na kile, inachukua miaka mingi.
Hakuhitaji kujifunza kwanza herufi na matamshi. Pale pale alianza kuzungumza. Huo ni uwezo wa kipekee sana.
Ndiyo maana Mungu alipomwumba Adamu, alimletea wanyama aangalie majina ya kuwapa. Pale pale, wote, Adamu aliwapa majina (Mwanzo 2:19-20).
Kwa hiyo Adamu aliumbwa na lugha tayari kichwani ambayo kwa kupitia hiyo angeweza kuwasiliana na mkewe, wanawe pamoja na Mungu.
Lugha hiyo Adamu aliyoumbwa nayo ni wazi kuwa iliendelea kutumika kwa vizazi na vizazi, hadi wakati wa Babeli, ambapo lugha nyingi ndipo zilipozaliwa (Mwanzo 11).
Kuitambua lugha yenyewe hasa ni ipi, ni vigumu.
Inawezekana ni moja ya lugha tunazotumia hivi leo, au ilishamezwa ndani ya lugha nyingine na kupotea kabisa.
Hata hivyo, kulingana na tafsiri za mila za Kiyahudi, ambapo jina ADAMAH maana yake ni udongo, inakisiwa kuwa huenda lugha hiyo ilikuwa ni KIYAHUDI.