Advertise here

Unapochagua mtu wa kuishi naye moja ya kitu muhimu kutambua ni kwamba ili familia yenu istawi na kufika mbali zaidi kimafanikio lazima

Kasomi

JT Founder
Anaandika Emmanuel Minga

Unapochagua mtu wa kuishi naye moja ya kitu muhimu kutambua ni kwamba ili familia yenu istawi na kufika mbali zaidi kimafanikio lazima

1::mmoja wenu awe ni mtu aliyebeba maono( mara nyingi huwa ni mwanaume) mtu aliyebeba dira na mwelekeo wa kule familia inatakiwa kufika.

Huyu ndiye aliyebeba ramani ya vile familia inapaswa kuwa.

Huyu ni muhamasishaji na mtoa support kwa upande wa maelekezo, maagizo na fedha.
Huyu ni kama kiongozi anayesimamia kila kitu kwamba kipo sawia.

Huyu ni muhakikishaji ulinzi na mambo mengine yote kuwa yapo sawa. Huyu ni mlipaji wa gharama kuhakikisha rasilimali zote za kuzalishia matokeo zinapatikana.

2:: mwingine awe mwepesi sana kuelewa na mtendaji wa haraka, mtu anayeweza kufikiri kwa undani na kwa haraka zaidi ( mara nyingi huwa ni mwanamke)

Huyu kazi yake ni kuzibadilisha rasilimali ziwe matokeo yanayotakiwa.

Huyu huangalia kila eneo ambalo halipo sawa na kutoa mawazo kile angetamani kifanyike ili hicho kitu kiwe sawa. Huyu ni mborshaji na musababisha ubora.

Huyu ni mtu mwepesi sana kugundua tatizo hata wakati mwingine kabla halijatokea.

Huyu ndiye mtekelezaji mkubwa wa mipango yote ya familia.

Huyu ndiye anayejua mahitaji yote na vitu vyote vinavyohitajika na vinavyofaa kwa familia.

Hii ni nguvu ya utendaji na ni mtu anayetamani aone matokeo hii ndiyo furaha yake.

Huyu ananguvu ya kulea maono na yakatokea kweli.

Note::mtu wa kwanza akikosa mtu wa pili hakuna kitakachoendela na vivyohivyo mtu wa pili akikosa mtu wa kwanza hakuna kitakacho endelea.

Hivyo ni muhimu kulitambua hilo,

Na ukiona mtu wako hayupo hivyo ukiona vyema unaweza kumtengeneza kuwa hivyo, kuna hatua kadhaa za kuzifuata na baadaye atakuwa mtu wa ndoto zako.

Nakupenda

E.M✍️
 

Similar threads

Back
Top