Kasomi
JT Founder
Hapo jana siku ya tarehe 3/4/2022
Watu kadhaa wanahofiwa wamefariki dunia baada ya kutokea ajali iliyohusisha basi lijulikanalo kwa Jina la Geita Express kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 134 DXR katika eneo la Chinangali II Mkoani Dodoma.
Habari zaidi zinafuata.
====
Watu wanne wamefariki na wengine 19 kujeruhiwa katika ajali ya basi la GEITA EXPRESS namba T 640 DLE linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Geita baada ya kugongana na gari namba T 134 DXR Fuso katika kijiji cha Manchali Chamwino mkoani Dodoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Onesmo Lyanga akiwa eneo la tukio ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa gari aina ya fuso kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.
Amesema majeruhi katika ajali hiyo wamefikishwa katika hospitali ya Uhuru wilaya ya Chamwino na wanaendelea kupatiwa matibabu.