Advertise here

Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo

Kasomi

JT Founder
1750709173948.jpg

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU

Dar es Salaam 23 Juni, 2025

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho na mabadiliko ya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi waliohamishwa na walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-

A: Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa

1. Mhe. Kenan Laban Kihongosi amehamishwa kutoka Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha; na

2. Mhe. Anamringi Macha amehamishwa kutoka Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

B: Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa

1. Balozi Simon Nyakoro Sirro ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma;

2. Mhe. Kheri Denice James ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa;

3. Mhe. Mboni Mohamed Mhita ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga;

4. Mhe. Beno Morris Malisa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya; na

5. Mh. Jabiri Omari Makame ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe

=======
Hapa Chini ni uchambuzi wa teuzi hizo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha akichukua nafasi ya Paul Makonda.

Kabla ya Uteuzi huo, Kihongosi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe, Beno Morris Malisa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mhe. Mboni Mohamed Mhita kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Kheri James kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Kabla ya uteuzi huo Sirro alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemhamisha Mhe. Anamringi Macha kutoka Mkoa wa Shinyanga kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
 

Similar threads

Back
Top