Kasomi
JT Founder
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, leo August 27, 2025.
Itakumbukwa jana Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kiliomba kukutana na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dharura ili kimuwasilishie maoni ya Wadau mbalimbali juu ya changamoto ambazo zinapaswa kutatuliwa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ili kulifanya Taifa kuingia kwenye uchaguzi likiwa na amani na kurejesha imani ya Wananchi kwenye Mamlaka za uchaguzi.
Akiongea na Waandishi wa Habari jana August 26, 2025 Jijini Dar es salaam, Rais wa TLS Boniface Mwabukusi alisema “TLS imewasiliana na Ofisi ya Rais ili kuwasilisha maazimio ya Wadau, tukipata nafasi ya kukutana na Rais, tutatoa ushauri wa hatua za haraka za kuchukuliwa ili kurudisha imani ya Wananchi na kuhakikisha uchaguzi unakuwa shirikishi, shindani na wenye uhalali wa kisiasa”
“Hadi hivi sasa hatujapata majibu kutoka Ofisi ya Rais ila kuna umuhimu wa TLS kuwasilisha maoni hayo, tunayo nafasi ya kusimama imara kama Taifa kwa kusikilizana na kuelewana kwenye masuala muhimu ya kitaifa kama suala la uchaguzi mkuu”
Chanzo: MillardAyo