Kasomi
JT Founder
Karume day ni siku ambayo huazimishwa kila ifikapo tarehe 07/04 kila mwaka kwa Tanzania nzima (Bara na visiwani).
Je, karume ni nani?
Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi.
Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
====
ABEID AMANI KARUME alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar.
Alizaliwa mwaka 1905 na akafariki mwaka 1972 tarehe 7 April kwa kupigwa risasi.
Aliiongoza Nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultan aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi 1964.
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na J.k Nyerere.
Baada ya Muungano huo ikazaliwa Tanzania.
KARUME alikuwa makamu wa kwanza wa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
AMAN ABEID KARUME mtoto wa Sheikh Karume alikuwa Rais wa Zanzibar tangu mwaka 2000- 2010.